Klabu ya Simba imeweka rekodi ya kuwa miongoni mwa klabu za Afrika ambazo zinaongoza kwa kuwa na wafuasi wengi katika Mtandao wa Kijamii wa Instagram na kuzifunika nyingine kongwe zikiwemo TP Mazembe ya DR Congo na Esperance ya Tunisia.
Simba imefi kisha wafuasi (followers) milioni moja katika mtandao huo na kuungana na klabu ya Zamalek ya Misri ambayo ina wafuasi milioni 1.3 huku klabu ambayo ina wafuasi wengi ni Al Ahly ya Misri iliyofi kisha milioni 4.9.
Mazembe ambayo inachezewa na Watanzania Eliud Ambokile na Ramadhan Singano ‘Messi’, ina wafuasi 24,000 (24.7k), Kaizer Chief 466,000 (466k), Orlando Pirates 229,000 (229k), Esperance 215,000 (215k) na AS Vita 26,000 (26k).
Nyingine ni Wydad Casablanca 43,000 (43k), Mamelodi Sunbdowns 163,000 (163k), Al Masry 135,000 (135k), Asec Mimosas 22,000 (22k), Zesco United 58,000 (58k), Asante Kotoko 10,000 (10k), Gor Mahia 29,000 (29k), Yanga 429 (429k) na Azam 246,000 (246k).
0 COMMENTS:
Post a Comment