December 18, 2019


Uongozi wa klabu ya Yanga umetuma kikosi kazi nchini Uganda kumfuatilia straika wa timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’, Fahad Bayo kwa ajili ya kupata saini yake katika usajili wa dirisha dogo linalotarajiwa kufunguliwa wiki ijayo.

Uongozi wa Yanga upo katika mchakato wa kuboresha kikosi chake baada ya nyota kadhaa wa kimataifa akiwemo Lamine Moro, Juma Balinya, Sadney Urikhob kutokuwa sehemu ya kikosi hicho kwa sasa huku wachezaji wengine kama Suleiman Mustafa, Issa Bigirimana na Maybin Kalengo wakiwa njiani kuachwa katika kikosi hicho.

Hata hivyo, ukiachana na mchakato huo wa usajili unaoendelea kuna wachezaji wanne wa kimataifa kutoka Malawi, DR Congo na Eritrea, wametua kwa ajili ya kufanya majaribio kikosini hapo.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa kamati ya ufundi ya Yanga imetuma watu maalum katika michuano ya Cecafa kwa ajili ya kuangalia wachezaji wenye viwango ambapo tayari wameshafanikiwa kuanza mazungumzo na Fahad.

“Mchakato wa usajili unaendelea kama ulivyopangwa, kuna watu maalum ambao wameteuliwa kwa ajili ya kwenda kufuatilia michuano ya Cecafa kwa ajili ya kwenda kuangalia vipaji vya wachezaji katika michuano hiyo ili kupata nafasi ya kusajili wale ambao wataonekana wapo vizuri.

“Hadi sasa tayari kuna mshambuliaji wa Uganda, Fahad ambaye wajumbe waliokwenda kule wanafanya nae mazungumzo ya awali, hivyo mipango ikikamilika tutamsajili.

“Lengo letu ni kuboresha kikosi chetu katika nafasi ya mshambuliaji mmoja, viungo wawili, beki wa kushoto na beki wa kati mmoja, kuhusu wachezaji ambao tatawafungashia mikoba wapo, tunasubiria dirisha la usajili lifunguliwe ndipo tuweze kuwaweka wazi,” alisema Bumbuli.

Yanga inaonekana kuweka nguvu kusajili mshambuliaji kwa kuwa wamekuwa na tatizo la uhaba wa mabao katika michezo yao ya hivi karibuni, hivyo straika huyo anayeichezea Vipers S.C inayoshiriki Ligi Kuu ya Uganda anaonekana kuwa anaweza kutatua matatizo yao.

3 COMMENTS:

  1. Inaingia akilini baada ya nyota Balinya teye mwenyewe na wengineo wengi kuonda kuvunja mikataba Yao kwa kukosa malipo Yao Bila ya kuwatonya Waganda wenziwe yaliyomfika yeye na wenziwe?

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwani hujawahi ona/sikia demu kamuacha jamaa kwa ukata,lakini akatokea demu mkali zaidi kutoka mtaa huohuo na kuja kwa jamaa na maisha yakaendela...!Walioachwa/kuvunja mikataba wote wana viwango duni, mbona hujamsikia shikalo,sibomana,Tshishimbi wakilalamika hawajalipwa...za kuambiwa changanya na za kwako

      Delete
  2. Yap, yani ni sawa na unasikia mahali fulani au nchi fulani kuna njaa halafu na wewe unakwenda, wachezaji hawalipwi mishahara miezi miwili mpaka wanagoma, lamine analipwa mshahara na GSM na hao wengine watalipwa na kina nani, pia sijui hata kama wanajua maana na dirisha dogo, dirisha dogo ni la kujazia sio kusajili timu nzima, maana yake ni kuwa hao wapya mpaka waelewe soka au ligi ya bongo ligi imeisha na hali ni mbaya. Ya ngoswe tuna waachia ngoswe wenyewe....

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic