Kuna uwezekano mkubwa mshambuliaji mpya wa Yanga, Ditram Nchimbi, anaweza asiwe sehemu ya mchezo dhidi ya watani wa jadi Simba, Januari 4 2020.
Yanga ilimtambulisha mchezaji huyo ambaye alikuwa kwa mkopo Polisi Tanzania wakati akiwa ana mkopo na Azam kwa kuingia naye mkataba.
Taarifa zinasema kuwa mabosi wa Polisi Tanzania wametuma barua kwenda TFF wakieleza kuwa kuna makubalinao maalum waliingia na Azam baada ya kumchukua kwa mkopo.
Polisi wanadai kuwa makubaliano hayo ni kama yamekiukwa mpaka imepelekea Nchimbi akaelekea Yanga kitu ambacho wao wanadai kuna baadhi yamekiukwa.
Kinachosubiriwa hivi sasa kwa TFF ni kutoa tamko juu ya Nchimbi ambaye kama mambo hayatakuwa sawa anaweza kuikosa mechi dhidi ya Simba.
Yanga huu mwaka wenu mmebanwa kwenye corner
ReplyDeleteTunajua matola ashaanza kujinyea na kujifanya anajua vipengele vya mikataba ya nchimbi na polisi na azam. atulie dawa isukumwe
ReplyDeleteYatakwisha hayo,viongozi wapo na nia yao kurejesha furaha jangwani.
ReplyDeleteYanga bhana! Hivi huyo Nchimbi mnamuona wa maana kwa kuwa tu aliwatungueni 3? Mbona ni mchezaji wa kawaida sana? Angekuwa mzuri kihivyo Azam FC wasingemuachia kirahisi hivyo.
ReplyDeleteunajua timu zet hazina maskauti wazuri kwa wachezaji. yaani namna nchimbi anavyoandikwa sasa ni kama vile hakuwahi cheza hapa bongo. mchezaji wa kiwango cha kawaida sana, kazunguka vitimu vidogo uwezo wake unaeleweka ni homa ya vipindi. sema kuwa miez hii ameonekana kuwa vizuri sasa ndio kila kona nchimbi nchimbi. na hii yote ni kwa ajili ya makocha kukosa elimu ya scouting na kazi hii kwetu huku inafanywa na viongozi, kisa nchimbi kaifunga yanga 3 basi anapapatikiwa, kisa yondani alimtaja mwamyeto kuwa ni mzuri na ngependa kuwa nae, yanga tayari wakamanza kumuwinda, simba ilipoona hivyo wakampa mkataba kwa kuwa kwao hela si tatizo. yule aliyewafunga ligi ya mabingwa wa ud songo, simba wakaona isiwe shida wanasajili. hivi yule ni bora kuliko okwi?
Deleteleo baada ya matola kuona nchimbi anaweza wasumbua na kwa kuwa TFF ni pacha na simba wanajivunia na wanajua Karia lazima apige pini.
kila la kheri,
karia Piga pini zuiya wachezaji wote wanaosajiliwa na Yanga hadi mechi ipite ili tuwafunge magoli ya kihistoria na iwe kumbukumbu kwa kizazi kijacho .
ReplyDeletekick za mchimbi ni kama za salamba tu,hao ni mastaa wa timu ndogo kama polisi tz,lipuli,namungo N.K
ReplyDelete