December 30, 2019


Uongozi wa klabu ya Yanga umefunguka kwa kusema kuwa kiungo wake Haruna Niyonzima, anatarajiwa kutua Dar es Salaam leo Jumatatu.

Kwa mujibu wa Ofisa Uhamasishaji wake, Antonio Nugaz, ameeleza kuwa mchezaji huyo atawasili nchini leo kujiunga na wenzake.

Nugaz amesema Niyonzima amechelewa kutokana na kutokamilisha baadhi ya masuala ya uhamisho baina yake na AS Kigali ambayo ilikuwa timu yake.

Ameeleza kwa kuwataka wanayanga wala wasiwe na wasiwasi sababu mchezaji huyo yupo njiani na anatarajiwa kutua kuanzia leo.

1 COMMENTS:

  1. Watani harakisheni ili awahi mechi ya 4.1.2020.Kila la kheyr

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic