LIGI kuu
Bara inazidi kupamba moto na ushindani unazidi kuwa mkubwa kwa timu shiriki
kutokana na ukweli kwamba kila timu inahitaji kupata matokeo chanya.
Kwenye
kutafuta matokeo tumeona kwa sasa bado mwamko wa mchezaji namba kumi na mbili
unazidi kuanguka siku hadi siku jambo ambalo halileti afya kwenye maendeleo ya
soka.
Ni wakati
muafaka wa mashabiki kujitokeza kwa wingi viwanjani kushuhudia timu zao
zinapocheza jambo ambalo litaongeza morali kwa wachezaji.
Kuna baadhi
ya mechi tunaona kabisa zinakosa mashabiki wa kutosha yaani wanakuwa ni wachache wa
kuhesabu kabisa kwenye majukwaa yote jambo ambalo sio jema kwa timu.
Muhimu
kujitokeza viwanjani kuwapa sapoti wachezaji kwani uwepo wa mashabiki ni muhimu
na kunafanya wachezaji kucheza mechi za ushindani.
Mechi nyingi
zinazochezwa kwa mfano nje ya mkoa wa Dar zimekuwa hazina ule mwamko mkubwa wa
mashabiki licha ya timu kucheza nyumbani.
Tunaona timu
kama Mbeya City ambayo inakwenda mwendo wa kusuasua imekuwa ikipata mashabiki
wachache kwenye mechi zake nyingi za nyumbani hii pia huenda ni sababu kwa
kiasi chake kwa timu kuboronga.
Wachezaji
wanashindwa kujua iwapo wapo watu ambao wanawafuatilia hakuna anayewashangilia
wala kuwazomea pale wanapochemka inaua morali kwa kiasi chake.
Kuna umuhimu
mkubwa wa sapoti kwa mashabiki kujitokeza viwanjani kwani kwenye mpira kila
mmoja ana umuhimu wake.
Hata timu za
Dar pia hakuna timu yenye uhakika wa kupata mashabiki wengi kutokana na mwamko
kuwa mdogo rai yangu kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi.
Mchezo wa Jumatau ya wiki hii uwanja wa Taifa ambapo Yanga ilikuwa inacheza na KMC bado mashabiki
hawakuwa wengi licha ya matangazo kufanyika.
Wengi
wamekuwa wakikimbilia kwenye vibanda umiza hii sio tabia nzuri hasa kwa wale ambao
wapo karibu na uwanja na wanaweza kufika.
Kwa wale
wenye uwezo wa kufika uwanjani wanapaswa wafike ndani ya uwanja na kutoa sapoti
kwa timu yao ila wale ambao wapo mbali basi itapendeza wakitazama kupitia
vibanda umiza.
Kumeanza
kuskika kelele kwamba waamuzi wanashindwa kufuata sheria 17 za mpira kutokana
na presha kuwa kubwa ndani ya ligi pia hata kule kwenye Ligi Daraja la Kwanza.
Katika hili
mamlaka husika, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linapaswa lisipuuzie
malalamiko haya na kutazama kuna jambo gani ambalo linaendelea katika hili.
Tumemskia
kocha wa Yanga, Boniface Mkwasa naye akizungumzia hili baada ya kupata sare ya
kufungana bao 1-1 mbele ya KMC na kudai kwamba pambano liliamuliwa na mwamuzi.
Ili ligi iwe
bora kila mmoja anapaswa awe makini katika kutimiza majukumu yake mwanzo mwisho
ili kuendeleza ubora wa ligi yetu ambayo inafuatiliwa na watu wengi.
Ni jukumu la
kila anayepewa mamlaka kufanyia kazi kwa usahihi kile ambacho anakifanya bila
kumuumiza mtu, nina amini kila kitu kitashughulikiwa na mambo yatakuwa sawa.
Kwa upande
wa ratiba imekuwa bado haieleweki namna inavyopangwa na kupanguliwa pia katika
hili bodi ya ligi kuna umuhimu wa kulitazama hili.
Azam FC nao
pia mechi yao ya hivi karibuni walilazimisha sare ya kufungana mabao 2-2
inaelezwa kuwa ratiba awali ilikuwa mechi ichezwe saa moja usiku mwisho wa siku
ikabadilishwa na kupelekwa majira ya saa 10 jioni.
Suala la
kubadili muda ama ratiba halikatazwi ila kikubwa ni kwamba ni wakati gani
mabadiliko yanafanywa na ni nani ambaye anahusika katika mabadiliko hayo.
Dunia nzima
imemshuhudia nahodha wa Azam FC, Agrey Morris akiongea kwa uchungu namna
anavyoona timu yake haijatendewa haki kwa kubadilishiwa muda wa kucheza mchezo
wao.
Anaeleza
kuwa walipewa muda mfupi kabla ya mechi jambo ambalo limewapotezea dira na
kupata sare ya kufungana mabao 2-2 wakiwa nyumbani Chamazi mbele ya JKT
Tanzania.
Katika hili
pia ni muhimu kuweka mpangilio mzuri kuepuka zile panga pangua za ligi ili
kuona kwamba kila timu inapata muda wa kujiandaa vema na kupata matokeo ambayo
wanayahitaji.
Jambo la
msingi ni kuona kwamba ligi yetu inakuwa bora kuliko jana katika kile ambacho
kinaendelea kwani hizi ni kazi za watu na wanategemea kupata ugali kwenye
mpira.
Imani yangu
ni kwamba mabadiliko yanawezekana katika hili iwapo kila mmoja hatabahatisha
katika kile anachokifanya matokeo yataonekana.
Ubabaishaji
muda wake kwenye soka umeisha ila kwa sasa ni lazima tukubali kwamba teknolojia
imekuwa na kila kitu kipo wazi.
Jambo la
msingi pia kwa wachezaji ni kutosahau majukumu yao kwa sasa kwani kuna baadhi
ya timu ambazo zipo mapumziko na nyingine zinaendelea kupambana na mechi zao.
Wakati mzuri
wa kujiaandaa kwa timu ambazo hazitakuwa na mechi kwa sasa na kuona namna gani
zitafikia malengo ambayo wamejiwekea.







Waswahili wanasema kumpigia gitaa mbuzi
ReplyDeletejkt wanatoka nnchi gani mbona wao hawalalamiki kubadilishiwa muda?
ReplyDelete