Uongozi wa klabu ya Yanga umesema utalitolea ufafanuzi wa kina suala la wachezaji wake wa kigeni kuondoka klabuni hapo.
Juzi zilienea taarifa za wachezaji Lamine Moro, David Molinga, Juma Balinya na Sadney Urikhob kutangaza kuachana na timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga, Kariakoo.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu, Hassan Bumbuli, amesema watalitolea ufafanuzi wa kina leo na akiwataka wanayanga kutulia akisema kila kitu kitakuwa sawa.
Bumbuli ameeleza wataeleza kila kitu na mustakbali mzima wa wachezaji hao ambao wametekea vyombo vya habari katika medani za soka hivi sasa.








Walipwe chao tatizo kumalizika wala haihitaji ufafanuzi wowote
ReplyDeleteKwani tatizo ni ufafanuzi au madai yao siyo stahili?
ReplyDeletewalipeni UFAFANUZI mumalize shida zo
ReplyDeleteSASA TUMEJUA SABABU YA KUFUKUZWA ZAHERA , WALISHAJUA KUA SIKU HII ITAFIKA NA ZAHERA ATAPASUA UKWELI WOTE BILA CHENGA - SIJUI UBABAISHAJI UTAISHA LINI KATIKA VILABU VYETU .
ReplyDeleteAlmuradi kila mmoja anachochea moto wake na huku kusajili dirisha dogo. Mambo hayaingii akilini hata kidogo Jee na Hao waliokubaliwa kuondoka kweli itakuwa salama Bila ya kudai chao
ReplyDeleteMabadiliko ya Uendeshaji na kuifanya timu kuingia kwenye uwekezaji .....NINASHANGAA M/KITI ANASEMA ILE KAMATI ILIYOUNDWA INAENDELEA NA MCHAKATO KUTOKA MWAKA JUZI IMEKUWA NA VIKAO VINGI SANA YAANI WANASEMA MPAKA MWAKANI MWEZI WA 6....SASA WATAKUWA WAMECHUKUA MWAKA. 1 1/2...HUKU MNALIA GHARAMA ZA UENDESHAJI NA MAPATO HAYALINGANI NA MATUMIZI........MNATEGEMEA KUONGEZA WANACHAMA KUANDIKISHA WANACHAMA ILI MPATE FEES ILI ZIENDESHE KLABU KUBWA KAMA YANGA??? DAWA NI KUINGIA UBIA/UWEKEZAJI NDANI YA SIKU 60 HAKUNA MUDA WA KUSUBIRI KWAKUWA MMESHAPOTEZA MUDA MWINGI KATIKA MICHAKATO....KUNA VITU VINATAKIWA MITAJI MIKUBWA YA FEDHA KAMA USAJILI, KAMBI, POSHO, UJENZI WA VIWANJA VYA MAZOEZI (KIGAMBONI & KAUNDA) AMBAPO NI MATAJIRI WENYE UWEZO WA KIFEDHA WANAWEZA KUTATUA HILI.....MSIWE NA MAWAZO YA KARNE YA 18...KUTAFUTA MICHANGO KUTOKANA NA KUINGIZA WANACHAMA WAPYA HIZO NI NDOTO HAMUWEZI KUFANIKIWA...100% WANACHAMA KULIPA MICHANGO HAWAWEZI.....KUTOKANA NA UHALISIA WA UCHUMI UNAOBADILIKA KWA KASI
ReplyDelete