Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa zoezi la usajili wa wachezaji wapya ndani ya kikosi chao utamalizika rasmi Jumanne ya wiki ijayo.
Mpaka sasa mabingwa hao wa kihistoria kunako Ligi Kuu Bara wameshakamilisha usajili wa nyota watano.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu, Hassan Bumbuli, amesema zoezi lao la usajili litakamilika Jumanne na akiwataka mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kuendelea kuwa watulivu.
"Niwaambie tu kuwa zoezi la usajili wa wachezaji wapya klabuni kwetu litaisha Jumanne.
"Tunasajili wachezaji ambao wana uwezo na wanaweza kuleta changamoto kwa wapinzani."
Kwa upande mwingine, Ofisa Mhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz, ameeleza kuwa usajili wa sasa ni wa rasharasha huku akiahidi mziki kamili bado unakuja.
Simba mwenda kimya Bila ya kelele nyingi ndie Simba mla nyama. Furaha haitokani na usajili bali inatokana na ushindi. Unaweza Kununuwa Gari la fahari lakini ukashidwa kulitunza. na kimya kikuu kina ushindi mkuu
ReplyDeleteMtamaliza misemo yote ila kwenye mioyo yenu wana simba lazima kutakuwa na hofu hasa kuelekea kwenye game ya watani hio tar4,na kibaya zaidi kwenu ni kwenda kwenye mchezo huo huku mkiwa na mwalim mpya ambae hajawah kukutana na daby ya aina hio......labda hio mechi aachiwe matola na mwalim mkuu akae pembeni
DeleteMwalimu ni mwalimu huwa haekezwi jinsi ya kushika chaki. Tarehe 04/01/2020 siyo mbali brother
ReplyDeleteyebo yebo tulieni hii c ndondo cup,tar 4 sio mbali
ReplyDeleteHiyo siku ya siku mtatokea kwa milango ya nyuma kumkimbia nyama aliyeshiba
ReplyDeletehuyo pimbi anaesema mwalimu mpya ina maana mkwasa amekaa na hyo timu muda gan? tumia akili
ReplyDeleteMlipofungwa goli 6 alikuja mwalimu Samsanov kutoka Bulgaria. Mgeni mkasema hivyo hivyo. Goli 6 zikatinga. Tarehe 4 sio mbali.Bado wiki 2 ndio mwisho wa Mkwasa kuwa kocha.
ReplyDelete