Yanga imefanya maamuzi magumu kwa kuwapukutisha mastaa watano wa kigeni akiwemo Sadney Urikhob ambae amewawahi kwa kuandika barua ya kuvunja mkataba. Jumamosi iliyopita kwenye mitandao ya kijamii zilisambaa habari za wachezaji kadhaa wa Yanga kuvunja mikataba kwa madai kwamba hawajalipwa mishahara kwa miezi mitatu.
Habari za uhakika ambazo Spoti Xtra imezipata ndani ya Yanga jana ni kwamba wachezaji hao wanadai mishahara ya Oktoba na Novemba lakini jana viongozi walikuwa wanakwepa kutoa ufafanuzi rasmi licha ya presha ya mitandaoni.
Chanzo makini ndani ya uongozi kimelithibitishia Spoti Xtra kwamba wamepanga kuachana na wachezaji watano wa kigeni ambao wamekuwa ni mizigo kwa klabu. “Mishahara siyo miezi mitatu, ni kweli wanadai lakini ni Oktoba na Novemba tu, Desemba si ndio kwanza imeanza? Utauhesabiaje?” alihoji kiongozi huyo na kuongeza.
“Hizi vurugu za wachezaji kuna baadhi ya watu wanaichochea kwa makusudi kabisa lakini sisi tayari tulishajua nani tunamuacha na karibu wote wanajua, hao wanaozungumza mitandaoni wote wanajua wanaachwa na barua zao wanazo.”
Kiongozi huyo alisema kwamba Yanga imepanga kuwatema wachezaji watano wa kigeni ambao wameona hawana faida nao kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao ndani ya uwanja kwa mujibu wa mikataba.
Aliwataja wachezaji wanaobaki kuwa ni David Molinga, Patrick Sibomana, Lamine Moro, Papy Tshishimbi na Farouk Shikhalo. Wanaotemwa kutokana na majeruhi na viwango ni Sadney Urikhob, Juma Balinya, Maybin Kalengo, Issa Bigirimana na Mustafa Suleiman.
“Mtu kama Kalengo na Bigirimana tumeshawaambia muda mrefu kwamba hatutakuwa nao kutokana na hali zao na viwango vyao, huyo Sadney na yeye pia tulishamwambia alichofanya ni kukimbilia kwenye mitandao kujikosha kwa vile aliona akitangazwa atadhalilika.
“Hao wengine ishu za mishahara tutamalizana nao tu kwa vile kuna mambo mengi tulikuwa tunayaweka sawa, safari hii tutasafisha sana timu usajili mkubwa wa Zahera (Mwinyi) utaondoka,” alisisitiza kiongozi huyo.
Habari zinasema kwamba Yanga waliisuka mikataba ya wachezaji wengi kiakili ili wasije kulipa fidia kubwa na wachezaji wengi wanaoondoka wamenasa kwenye kifungu cha uwajibikaji.
Licha ya kwamba baadhi ya viongozi wanadaiwa kuwa upande wa wachezaji hao wanaoshinikiza kulipwa stahiki zao, habari zinasema kwamba hata kwenye wachezaji wa ndani litapita panga ambao watano au sita watapelekwa kwa mkopo kwenye timu zingine ikiwemo Singida United.
Miongoni mwao ni beki mfupi, Mwarami Isa ‘Marcelo’ na Ally Ally. Dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu Bara linafunguliwa Desemba 16 na kufungwa Januari 15, mwakani.
CHANZO: SPOTI XTRA








Kwani kina Lamine Molo, David Molinga hawakuwa wa Zahera? Siasa za kijinga katika mpira hazina nafasi muhimu waache uswahili na waweke weledi mbele ili timu yao iweze kukaa sawa. Je hao wataowaleta mambo yakikataa Zahera atakuwepo ili kiwe kisingizio?
ReplyDeleteViongozi wa mpira Tanzania aanapaswa kubadilika sana kwa manufaa ya mpira kwani inasemwa MPIRA NI MCHEZO WA WAZI. Inaanza kuaminisha kwamba Mwinyi Zahera alichokisema kuhusu uongozi huu kina ukweli mwingi kwamba wachezaji wengi aliletewa na alikuwa akiwalipa wachezaji fedha zake za mfukoni sasa njaa imezidi mambo yamelipuka huku viongozi waliuaminisha umma kwamba kutokana na udhamini mkubwa ambao timu imeupata hakuna njaa tena!! Je na Dante naye ni kingamizi la Zahera? Je awali kwanini hawakusema kama timu inadaiwa wakati bakuli la KUBWA KULIKO linatembezwa?
Ifike mahala viongozi wa mpira waache kuwafanya wajinga wale waliowapa dhamana ya uongozi katika hizi klabu zetu. Waseme ukweli na waache siasa za magazetini ili mpira wetu ukue.
Braza ukipapalika na taarifa za mitandao utakuwa unapotea. Waandishi wanataka habari zao zisomwe lakn kwa uhakika sikiliza wanachosema viongozi. Umeshwahi kujiuliza kwanini huwa mara zote taarifa huwa hazina uhalisia wa sauti ya kiongozi???basi baki upate kile kinachotakiwa. Ufanisi wa Lamine, Tshikalo, Molinga, Sibomana huwezi fananisha na wa Juma Balinya au Mustapha Suleiman. Tuache watu wafanye kazi
DeleteWell said......
DeletePia Hakuna mtu anayeizidi yanga wanayanga tunachotaka ni matokei huwezi sepa pisha wanaojua
ReplyDeleteUkweli utajulikana tu,viongozi watumie sana akili kuhusu hili la wachezaji kuondoka,washabiki ,wapenzi na wadau wanaangalia ni kitu gani kinachoendelea.
ReplyDeleteUko nikujificha ili mashabiki wasijue kinacho endelea lkn ukweli yanga wananatatizo makubwa sana
ReplyDelete