December 30, 2019


BIASHARA United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Francis Baraza kutoka mkoani Mara walibakiza dakika sita tu kuambulia pointi kwenye mchezo wa leo dhidi ya Yanga uliocchezwa uwanja wa Taifa ila bahati haikuwa yao walipoteza.

Bao pekee la ushindi kwa Yanga limefungwa na Tariq Seif dakika ya 84 akimalizia pasi ya nahodha Papy Tshishimbi akiwa ndani ya 18 na kuzamisha moja kwa moja wavuni.

 Seif ambaye aliwahi kucheza Biashara United kabla ya kusajiliwa hivi karibuni kwenye dirisha dogo ndani ya Yanga akitokea nchini Misri amesema kuwa anaona fahari kuipa pointi tatu, timu yake.

"Nimefurahi kuona nimeipa ushindi timu yangu inaamanisha kwamba ninaweza na nitaendelea kupambana kwa kushirikiana na wenzangu ili kuwa bora zaidi," amesema.

Yangaimecheza jumla ya mechi 11 inafikisha jumla ya pointi 24 sawa na Kagera Sugar inakuwa nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao ya kufungwa ikiwa nyuma ya Simba walio kileleni wenye pointi 31 wakiwa wamecheza jumla ya mechi 12.

12 COMMENTS:

  1. Kwa mpira huu siendi uwanjani tarehe 4.Sina ushujaa huo.Nitasikiliza kwenye redio.

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. Mimi Yanga lakini nakaa kimya. Timu yetu bado sana.Kujilinganisha kwa sasa mhhhhh.

    ReplyDelete
  4. wala sijapenda mchezo was Leo kabisa yan yanga tunakuwa tunabanwa namna hiyo kweli juma mos wala siangalii mtanipa matokei

    ReplyDelete
  5. mmeona gari la mkaa ni aibu tupu!

    ReplyDelete
  6. Tusipoangalia aibu inaweza kuwa KUBWA Jumamosi.Kocha akiingia kichwa kichwa kushambuliana na Simba itabidi tulale mapema.

    ReplyDelete
  7. Kwa Simba hii ya Moo hata ikifufuka Yanga ya Manji haki ya Mungu itagaragazwa kwa kichapo cha mbwa koko ikibweka pamoja na kutolipwa mshahara

    ReplyDelete
  8. Dk 84 ndio mnapata hako kabao kamoja poleni sana naona tarehe haifiki jamani

    ReplyDelete
  9. Naona kuna mtu ushindi wa yanga umemnyima raha anaandika comment Mara kumi bila support

    ReplyDelete
  10. Mbona wanaolalama ni vyura wenzako?Utaenda mpirani Jumamosi?Beba dawa za presha. Kipigo kirskuwa kikali.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic