Mabosi Yanga wamekamilisha dili la usajili la mshambuliaji wa Azam FC anayekipiga kwa mkopo Polisi Tanzania Ditram Nchimbi wakitumia kitita cha Sh Mil. 40 kufanikisha usajili huo.
Yanga ni kama wamewazidi ujanja Simba baada ya kufanikisha usajili wa mshambuliaji huyo aliyekuwa anawaniwa na klabu hizo kongwe katika usajili huu wa dirisha dogo uliofunguliwa juzi Jumatatu.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo tumezipata kutoka kwenye uongozi wa Azam, mshambuliaji huyo wamemuachia kwa dau hilo na kumtoa Polisi Tanzania alipokuwa anakipiga kwa mkopo.
Mtoa taarifa huyo alisema kati ya Sh Mil. 40, Azam imechukua Mil 20, huku mchezaji mwenyewe akichukua Mil 20 kama dau lake la usajili baada ya Yanga kuonekana kuvutiwa naye.
Aliongeza kuwa uongozi wa Yanga na Azam wamefikia makubaliano mazuri kwa pamoja kuvunja mkataba wake wa kuendelea kuichezea timu hiyo katika msimu huu.
“Nchimbi alionyesha nia kubwa ya kutaka kuondoka Azam ni baada ya yeye mwenyewe kuulazimisha uongozi ukubali kumuachia aondoke zake aende Yanga au timu nyingine lakini siyo kubakia hapo.
“Hivyo uongozi wa Azam haukutaka malumbano na mchezaji huyo na kufikia makubaliano ya pamoja kumuachia aondoke zake lakini kwa makubaliano ya kuuvunja mkataba kwa dau la Sh Mil. 20.
“Hivyo viongozi wa Yanga tayari wamesaini hundi ya Sh Mil. 20 na kuwapatia viongozi wa Azam huku ikibakia Mil. 20 ambazo hizo atapatiwa yeye kama dau lake la usajili,”alisema mtoa taarifa huyo.
Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla alikiri; “Leo au kesho (Jumatano) mwakilishi wetu kutoka Yanga atasafiri kwenda Uganda kwa ajili ya kwenda kumalizana na Nchimbi aliyepo kwenye kikosi cha Kilimanjaro Stars.”
YANGA iliizidi Simba kwa mfungaji bora wa Uganda Juma Balinya...☆¿# Acheni ujinga. Wazee wa bakuli wanaubavu kweli wa kushindana na kampuni kwa mchezaji wa kweli wanaemtaka? Yuko wapi mnambia?��
ReplyDeleteAcha povu kaka,simba mna kampuni gani na jina lake ni lipi,uwanja wenyewe tayari umekwisha itwa jina la Mo arena ndio mkae mkijua kuwa siku mtakapomuudhi tu anasepa na mali zake....
DeleteHizo ndio ndoto zenu chafu na ndio mana kila kukicha matatizo mapya. Moo kashamiri kwasababu hana hasadi
ReplyDeleteAcha povu kaka sasa ulitaka uwanja Simba uitwe jina gani? Mabakuli Arena? Huyo mchezaji mwenyewe Azam kawaingiza chakani.
ReplyDeleteWaandishi wetu wa habari ni wachonganishi na wazushi na wanawapumbaza sana watu....sasa hapa suala la Simba limeingiaje?
ReplyDeleteSimba kuna tatizo kubwa zaidi ya Yanga. Mmeolewa mmefanywa mama wa nyumbani. Mnacholetewa ndio mnachokula. Ata Manara hajui kwenye Akaunti ya Simba kuna shilingi ngapi. Ukiuliza vyanzo vya mapato vya simba watu hawavijui isipokuwa vile vya wadhamini uchwara ambao ata yanga wanavyo. Ukiuliza nani amemtafuta na kamleta kocha uongozi utakuambia sisi tumeletewa tu. Mtu mwenye akili timamu na uhuru wake hawezi kufurahia hali hiyo ata siku moja. Huwezi kwenda kushangilia uwanja ambao hujui umejengwa kwa fedha ipi. Haya mambo si ya kufanyiwa kizazi hiki cha wasomi ambacho mwalimu alitujengea shule ili tujitambue na kuondokana na hali ya kutegemea watu. Simba mnatudhalilisha mnapoturudisha enzi za mabwana na watwana.Najua ni vigumu kuwafungueni kwenye kifungo hicho. Ndio maana mwenyekiti mliyemchagua alipobwaga manyanga hamkujiuliza. HII NI AIBU KUBWA NA HASA PIA HUO UTARATIBU WENU WA KUNUNUA MECHI
ReplyDeleteUlichoandika dhahiri huna akili.
DeleteTunanunua mpaka vyura? Sasa ndio nimeamini ule msemo wa kila yanga 40 akili zao sawa mbuzi mmoja. Hivi matatizo ya simba ni makubwa kuliko yenu? Mlipeni dante kwanza tujue hamna shida. Kwa sasa mjilinganishe na national mgede ya mburahati med jongo sababu mnyama ameshatoka ktk mambo ya kudaiwa mishahara, na pia uwekezaji wetu ni wa kitaalamu na mikataba hivyo Sisi tunategemeana hatumtegemei ndio maana ya uwekezaji sio ufadhili. Akiondoka mo anaondoka yeye anakuja nyengine, kwahiyo vyura Rudini shule kidogo.
DeleteInawezekana kweli huyohana akili ila wewe ni zaidi ya huyo maana umeshindwa kumuelewa alichokiandika ila wenye akili walishamuelewa huyo
ReplyDeleteKwani Yanga na Simba inategemea watu? Simba ina muekezaji na Yanga inatembeza mabakuli kwa watu. Na kama vile haitoshi Simba ina mukezaji mzalaendo na tena kama vile haitoshi ni muekezaji Simba Damu yaani Simba asilia, kwa maana yakwamba hata Mo asiwe Muekazaji wa Simba basi ni mpenzi na mwanachama mketeretwa wa Simba huwezi kumuondoa pale pigine majungu mpaka ya kijinga mpaka mtoke kamasi. Simba ni kampuni na ina malengo na mukakati ya kujiendesha endelevu iliyowazi na kueleweka. Mfano viwanja vyao vya mazoezi kama moja ya utimilifu wa kati ya malengo waliyojiwekea Simba kunakokupiga hatua za kimaendeleo. Yanga hii kuifananisha na simba kiuongozi hata kihali ni sawa na kwenda kuigonganisha scania na bodaboda.Hata akili za mashabiki wa Yanga ni za kizezeta na ndio maana timu yao ipo ipo tu ikiendeshwa kihovyo hovyo tu .kinachoendelea Yanga ni kudhulumu wachezaji haki zao.Wapo wenye kulalamika na wakionekana maadui na wapo wale wa kigeni amabo kama kweli Yanga walilipa madau manono kuwasajili na kusepa zao bila kutoa huduma kwa klabu iliyotarajiwa basi hapo utaona uhovyo ndani ya Yanga. Mfano Juma Balinya,Sadney ukrihob,Mnyarwanda Birihiana,Kalengo wa Zambia ni wachezaji waliowatia YANGA madeni makubwa kwenye sajli zao lakini wote hao wanaondoka bila ya Yanga kufaidika na chochote sasa hapo kama mwana yanga unachekelea ujinga huo basi ujuwe akili zako bado zipo tete na ndio mnayoiyumbisha yanga .
ReplyDeleteTunakubali kuwa Yanga janja kuliko Simba yenye uwezo wa kila Aina zaidi ya ule wa Simba na ni timu iliyotulia bila ya mushkila na hayo ya madeni ni propaganda za wasiowatakia heri na ubingwa ni waoj
ReplyDeleteLini Simba walimtaka Nchimbi?
ReplyDeleteIli akacheze namba ngapi? Acheni habari za uzushi, mnapoteza hadhi. Hata Juma Balinya mlisema hivyo hivyo na kuwadanganya vyura eti mmewapora Simba mchezaji. Kiko wapi?