January 7, 2020

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa hauna mashaka na mchezo wao dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Januari 10, uwanja wa Gombani.

Azam FC ni mabingwa watetezi wa kombe la Mapinduzi walitinga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Obrey Chirwa mbele ya Mlandege FC.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa hawana mashaka watapambana.

"Sisi ni mabingwa watetezi hatuna mashaka na Simba kwani tuna uzoefu nao kwenye mashindano haya ya Kombe la Mapinduzi," amesema.

Simba ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Zimamoto, inafikisha jumla ya timu tatu ambazo zimetinga hatua ya nusu fainali ambazo ni pamoja na Mtibwa Sugar, zote za Bara.

2 COMMENTS:

  1. Huu ndiyo uandishi wa waandishi wetu wa Bongo. Headline na content ni vitu 2 tofauti!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic