January 12, 2020



KESHO, Visiwani Zanzibar, Uwanja wa Amaan, kutakuwa na mchezo wa kukata na shoka kati a Mtibwa Sugar na Simba ambao utakuwa ni wa fainali ya Kombe la Mapinduzi.

Mtibwa Sugar walikuwa wa kwanza kutinga hatua hiyo kwa ushindi wa penalti 4-2 walioupata mbele ya Yanga baada ya dakika tisini kulazimisha sare ya bao 1-1.

Simba nao walikuwa washindi wa nusu fainali ya pili mbele ya Azam FC kwa ushindi wa penalti 3-2 baada ya dakika tisini kutoka sare ya bila kufungana.

Azam FC ambao walikuwa mabingwa watetezi msimu huu watakuwa watazamaji wa fainali hii itakayopigwa Januari,13.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kutokana na timu zote kupania kutwaa taji la kwanza kwa mwaka 2020.

Kiungo wa Mtibwa Sugar, Humud amesema kuwa mchezo mgumu ulikuwa dhidi ya Yanga wana imani watapenya mbele ya Simba na kupata matokeo.

Kwa upande wa Simba, mlinda mlango, Beno Kakolanya amesema kuwa wachezaji wapo vizuri na wanaamini utakuwa mchezo mgumu ila watapabana kupata matokeo.

3 COMMENTS:

  1. mtibwa hii kwa simba hii watsubiri sana bado wachanga kuhili hiyo mikiki mikiki

    ReplyDelete
  2. Kwa mtibwa ninayoijua bado sana kuimudu simba ila nikujipa matumaini tu na kuvuta hamasa kwa mashabiki.kufungwa lazima tena mapema mnooooo,na wakifanya mchezo mtibwa watakula nyingi sana.

    ReplyDelete
  3. Mtibwa jaribuni kwa Mungu si makubwa kwani Nani alifikiria kuwa Mwadui Igeweza kumlaza Mnyama kwa goli moja

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic