Kaimu Kocha wa Yanga, Boniface Mkwasa, ameibuka na kusema kuwa hali yake kiafya hivi sasa iko salama kabisa.
Mkwasa ameamua kusema kutokana na baadhi ya wadau kuhoji juu ya usalama wa afya yake haswa baada ya kupewa nafasi ya kuifundisha Yanga akichukua nafasi ya muda kutoka kwa Mwinyi Zahera.
Ameeleza kuwa hana tatizo lolote kwa sasa tangu afanyiwe operesheni alipoenda kufanyiwa matibabu ulaya.
"Mimi niwatoe wasiwasi, kwa sasa nimepona kabisa, wale wanaosema naumwa basi niwahakikishie kuwa niko sawa.
"Hata tukienda kupima hospitali hii leo, najua wenzangu wanaweza kuonekana ni wagonjwa nami nishapona."
Kwa upande mwingine Mkwasa ametoa shukrani zake kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba, Zacharia Hanspope ambaye alikuwa ni moja ya watu waliompa sapoti wakati akiwa anaumwa.
Tunamshukuru sana Mungu kwa kumponya Mkwasa. Gazeti moja lilishafanya coverage yake ni mkewe slikiri kuwa mmoja wa viongozi wa simba walisupport, leo amemtaja great.
ReplyDelete