January 4, 2020


Leo Jumamosi gumzo ni mchezo wa Simba dhidi ya Yanga ambao unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kawaida kabla ya mchezo huo bila kujali ni wa mashindano au kirafiki huwa kuna presha kubwa kwa mashabiki na wachezaji.

Presha hiyo inatokana na kuzungumzwa na watu wengi, hasa kwa kuwa kwa levo ya soka la Afrika Mashariki ngazi ya klabu bado inaaminika ndiyo wenye upinzani mkubwa baina ya timu zinazotoka sehemu moja yaani derby kuliko klabu nyingine zote ukanda huo.

Kwa miaka mingi watu wengi wameshindwa kufika uwanjani kushuhudia mchezo baina ya timu hizo kwa kuwa tu kumekuwa hakuna mazingira rafiki ya usalama na burudani.

Hivyo basi ni muhimu kwa wasimamizi wa mchezo huo kuhakikisha suala la ulinzi na usalama linakuwepo kwa kiwango cha juu.

Wenzetu katika nchi zilizoendelea ni kawaida kuona idadi kubwa ya mashabiki ikijitokeza uwanjani, wake kwa waume pamoja na watoto, wote hao wanashiriki kwa kufika uwanjani kwa sababu kuna mazingira mazuri.

Hapa kwetu mara nyingi kunapokuwa na mechi kubwa suala la mazingira rafiki kwa mashabiki hasa ambao wanapenda kwenda na familia zao huwa ni utata, mara nyingi hiyo inatokana na kutokujipanga mapema.

Ni vema Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pamoja na Bodi ya Ligi wakashirikiana na wadau mbalimbali kutengeneza mazingira rafiki uwanjani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic