Uongozi wa klabu ya Simba umesema haujaachana na wachezaji wake Aishi Manula pamoja na Erasto Nyoni.
Kwa mujibu wa CEO mpya wa Simba, Senzo Mazingisa, ameeleza kuwa si kweli wameachana na wachezaji hao baada ya kuwa kwenye majeruhi hivi karibuni.
Akizungumza na Radio One, Mazingisa ameeleza bado wachezaji hao ni mali halali ya Simba na wataendelea kuwa nao siku zote.
Amefunguka kuwa wanaheshimu mchango wao na yanayoelezwa mitandaoni kuwa wameachana nao hayana ukweli wowote.
"Nyoni na Manula ni wachezaji wa Simba, hatujaachana nao kama inavyoelezwa.
"Sisi tutaendelea kuwa nao sababu kuwa majeruhi si chanzo cha sisi kuachana nao, yanayoandikwa yapuuzwe."
Wanaovumisha wanstaka kuwapa ahweni Yanga kuwa si peke Yao kuachana na nyota wao
ReplyDeleteIli iweje? Kwa kweli mambo ya timu nyingine kuongelewa kivingine haileti tija, shauri timu yako ijijenge vizuri
ReplyDelete