January 8, 2020


BARAZA la Sanaa Taifa (BASATA) limemtaka msanii wa Bongo Fleva, Tumaini Godfrey, maarufu Dudubaya, kufika katika ofisi za baraza hilo kesho Januari 7 (jana), kwa mahojiano zaidi baada ya kusambaa kipande cha video kikimuonyesha akitoa kauli zisizokuwa na maadili.

Hatua hiyo imo katika taarifa kwa umma iliyotolewana BASATA leo Januari 6, 2020.

Baada ya wito huyo, Dudubaya amejirekodi kipande cha video na kukirusha kwenye mtandao wa Instagram akisema:

“BASATA nimepata wito wenu na siwezi kuja, kwa sababu huwezi kuniita kuja kunionya kwa kurekodi clip za neno kufi… (tusi, kufanya ngono kinyume cha maumbile), hata mama Rwakatale kanisani huwa anasema kabisa kwamba wasagaji, walawiti wafi….(tusi)  hawataiona pepo.

“Hata katika vitabu vitakatifu Mungu hakufumba amesema kabisa kwamba walawiti wasagaji wafi…(tusi) hawataiona pepo, hata kama namfundisha mtoto wangu nitasemaje? Kufi….(tusi) ni vibaya, nimwambie kupigwa fimbo au?

“Lazima tuheshimiane, mkitaka nije lazima mhakikishe kwamba vyombo vya habari ambavyo vina ugomvi na wasanii, muweke suluhisho la amani ili muziki huu uweze kusonga mbele, siji,” amesema Dudubaya.

1 COMMENTS:

  1. Anamatatizo sana huyu jamaa,anajifanya yupo juu ya sheria,na anajiona ana haki ya kumsema vibaya na kumtukana kila mtu ambaye hapatani nae..anapaswa kubadirika pia akumbuke Sikio halizidi kichwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic