January 28, 2020


UONGOZI wa Simba umesema kuwa leo utalitolea ufafanuzi suala la madai ya mlinda mlango wa Yanga, Ramadhan Kabwili kudai kuwa aliahidiwa gari aina ya Toyota IST endapo angefanya makusudi ya kutocheza mchezo wao wa msimu uliopita 2018/19.

Kabwili alidai kuwa, kuna watu ambao anadai walikuwa ni viongozi wa Simba walimfuata na kumtaka afanye makusudi kwenye mechi zake apate kadi ya njano ili asipangwe kwenye kikosi kwa kuwa alikuwa na kadi mbili za njano.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa watajibu tuhuma alizotoa mchezaji huyo ila cha msingi awe na ushahidi.

" Tutajibu tuhuma za jumla jumla alizotoa huyu mchezaji kwa klabu yetu. Muhimu wakati huu akijiandaa kikamilifu na ushahidi wa hizo tuhuma," .

Shirikisho la Soka la Tanzania, (TFF) limetoa pia taarifa ya kusikitishwa na taarifa hizo kwa kuwa si mpango mzuri kwa maendeleo ya soka na wameahidi kulifanyia uchunguzi.

"Sektretarieti ya TFF imeiandikia barua Kamati ya Maadili kufuatilia jambo hilo ikiwa pamoja na kufahamu undani wa jambo lenyewe.

"Aidha TFF, itavijulisha vyombo vingine vya usalama ili viweze kuisaidia uchunguzi kubaini ukweli na hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

"TFF siku zote imekuwa ikipiga vita vitendo vya upangaji matokeo katika mpira wa miguu," ilieleza taarifa hiyo iliyotolewa na TFF kupitia Ofisa Habari, Cliford Ndimbo. 

12 COMMENTS:

  1. Ni madai mazito ila kijana ajiandae kwenda mahakamani kuthibitisaha madai yake.
    Anaposema viongozi wa Simba bila shaka ni wale viongozi wa Simba wanaojulikana kwa mujibu wa sheria. Kwa hivyo sidhani kama kabwili atakuwa na kigugumizi kutibitisha madai yake. Ila ni madai ya ajabu ni kana kwamba vile kabwili anajithibitishia kuwa ni kipa mkubwa na Simba walikuwa wanamuhofu lakini kiuhalisia Simba walimuhofu zaidi kindoki kuliko Kabwili na hata goli alilofungwa na Simba kunako mechi ile kama angelikuwa kindoki asingefungwa.

    ReplyDelete
  2. Kindoki hakua na ubora huo, tuache ushabiki

    ReplyDelete
  3. Kamata hao mikia, wamezoea kubebwa ndoo maana wanatolewa kwenye priminary stage!

    ReplyDelete
  4. What goes around....Simba mjitathmini sana. Mnaua mpira wa Tanzania. Mnatumia kila njia kuwadanganya wapenzi wenu Simba inashinda ili kuipandisha Brand ya Simba ili mpige hela na kufanya Biashara. Mpira unachezwa hadharani watu wanaona.

    ReplyDelete
  5. Kabwili angoje mwaka mzima kusema haya??Timing ya hili jambo ni kwa manufaa ya nani?Kwanini avunje sim card na ndio ilikuwa ushahidi?Timu zicheze mpira ziache majungu.

    ReplyDelete
  6. Simba wajitasmini,mana c mara ya kwanza hii itakua mara ya tatu km sikosei,mara ya kwanza simba walihusishwa kumpa rushwa dida pamoja na Agrey Morris, wa azam,tena ikapelekea hadi dida kutemwa na azam,la pili ilikua shabani kado,alisema kabisa kua simba walimtuma ulimboka akampe laki tano ili afungishe mechi na mtibwa,hili sasa la kabwili ni la tatu,mbona kila siku ni Simba tu,mbona azishutumiwi timu nyengine, hapo kuna kitu hata km utakosekana ushahidi lkn simba itakua na mchezo mchafu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha kuanza kutuhumu wote tupo gizani kila mtu anasubiri ukweli usiwe mjuaji sana na mwelewa kuliko hao wacha tuone mm mwenyewe naisubiri hii sinema, ni mechi ipi ambayo simba walishinda kwa kuonga wachezaji? je ni kweli kuwa kiwango cha Simba kinachokuwa kinaonyeshwa uwanjani ni cha kubebwa? bado sipati majibu kuhusu simba na sielewi. Tukana ukione maana mmezoea kutukana thubutu ugongewe mlango kuwa unahitajika.

      Delete
  7. Kwa hiyo hakupewa IST na bado akafungwa. Sasa si ni heri angeichukua tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuna mwingine walimpata. Ni campaign kubwa baada ya kuona mnakosa ubingwa kila mwaka

      Delete
  8. Dogo hawezi kuropoko kitu kisichokuwepo. Hatakosa ushahidi tu.

    ReplyDelete
  9. Kwani si kabwili huyu anaehusishwa na utonvu wa ndani ya Yanga? Sasa vipi ashindwe kuwa mzushi?

    ReplyDelete
  10. Alidai alimweleza kocha wake na kudai kocha alimshauri akomae hivyo hivyo. Kocha huyo Zahera kasema hayawahi kuambiwa kitu kama hicho alipohojiwa kuhusu tuhuma hizo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic