January 4, 2020



LEO uwanja wa Taifa, Simba itawakaribisha wageni wao Yanga kwenye mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara msimu huu wao kukutana Uongozi wa Simba umesema kuwa wachezaji wote wamepewa ujumbe maalumu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba Mohamed Dewji ‘Mo’.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema kuwa wachezaji wote wanatambua majukumu ambayo wamepewa uwanjani pamoja na ujumbe wa Mo kwenye mechi zao zote ikiwa ni pamoja na mchezo dhidi ya Yanga.

“Wachezaji wanatambua ujumbe ambao Mo amewaambia, ujumbe wake siku zote ni ushindi kwenye mechi zetu zote, kwa sasa klabu ya Simba ni kubwa kitaifa na kimataifa, kwa uwekezaji ambao tumefanya itakuwa aibu kupoteza kizembe jambo ambalo halipendezi kwa mashabiki na uongozi pia hasa linapokuja suala la mechi yetu dhidi ya Yanga.

“Uwekezaji ambao tumeufanya tunahitaji uwe na matokeo, hawa akina Kagere (Meddie), Shiboub (Sharaf), Bocco (John) wanatambua kazi yao hivyo mashabiki niwaombe kujitokeza kwa wingi kuona namna itakavyokuwa, nitaongea mengi baada ya dakika tisini,” alisema Manara.

Simba imecheza jumla ya mechi 13 ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 34 wapinzani wao Yanga wapo nafasi ya tano wakiwa na pointi 24 wamechea jumla ya mechi 11.

4 COMMENTS:

  1. Pika kandambili aka vyura wa jangwani

    ReplyDelete
  2. Leo ni goli 4 mnafungwa kandambili aka vyura wa jangwani

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mliwashindwa Prisons hapo Taifa mtawaweza Yanga?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic