January 15, 2020

BAADA ya Simba kulipoteza mara ya pili mfululizo Kombe la Mapinduzi kwa kupokea kichapo cha 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar hesabu zao zimebadilika ghafla na kuhamia kwenye ligi.

2019 Simba ilicheza fainali na Azam FC kwenye Kombe la Mapinduzi na ilichapwa mabao 2-1 na 2020 imeanza kwa kuchapwa bao 1-0 lililofungwa na Awadh Salum dakika ya 39 na kuwafanya wapoteze kwa mara nyingine tena.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kwa sasa mpango mkubwa ni kufanya vema kwenye mechi za ligi pamoja na mashindano mengine.

"Tumeumia kukosa kombe la Mapinduzi, ni matokeo mabaya kwetu ila hakuna namna maisha lazima yaendelee.

"Kwa sasa nguvu kubwa ni kwenye ligi pamoja na mashindano mengine lazima tupambane kufanya vema," amesema.

Simba kesho Januari, 16 itashuka uwanjani kumenyana na Mbao FC ya Mwanza, CCM Kirumba.

2 COMMENTS:

  1. Mbao baada ya hapo Alliance!!! Ondoeni mawazo ya Mapinduzi Cup turejee kwenye ligi ili tufunge midomo ya watu. Maana sasa kila kitu, kila siku hakuna habari nyingine zaidi ya GSM tuuuuuuu!!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic