January 16, 2020


Baada ya kupoteza kwa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa jana kunako Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, mchezaji wa zamani wa Yanga, Bakali Malima, amesema timu haikustahili kubadilisha kocha.

Malima ameeleza kuwa Yanga ilipaswa kuendelea kumwamini na kumtumia Mkwasa sababu tayari alikuwa ameshaanza kuwaweka sawa wachezaji kitimu.

Mchezaji huyo amefunguka akieleza kuwa Mkwasa alikuwa ameshaanza kuwapa somo wachezaji baada ya aliyekuwa kocha Mwinyi Zahera kuwaacha na walianza kuja vizuri lakini ameshangazwa na Yanga kumtoa Mkwasa.

"Unajua Yanga mimi nawashangaa sana kuleta kocha mwingine.

"Mkwasa tayari alikuwa ameshaanza kuwapa somo vijana na walianza kumwelewa, kwanini tena waachane naye na walete kocha mwingine.

"Sijaafiki, kuleta kocha mwingine kunazidi kuirudisha timu nyuma na ni maamuzi ambayo mimi sijayapenda."

3 COMMENTS:

  1. Maliama anaelewa maana ya kukaimu?

    ReplyDelete
  2. Kocha huyo mpya ni kama Zahera kutokana na ulalamikaji na majisifu, isipokuwa, Zahera alisaidia timu Sana ilipokuwa na matatizo ya mapato kwa kuisaidia timu kifedha au kuikopesha na kubuni njia za kuingiza mapato kwa kubuni michango kwa njia ya zungusha bakuli ambapo ilisaidia Sana. Jambo la ajabu pale Jana timu ilipokuwa inaelemewa vibaya, kocha badala ya kutoa taalimu kwa wachezaji yeye alikuwa akizozana na Benchi angalizi. Kocha huyo Ana mkataba wa mwaka na nusu. Mkwasa ilibidi a endelee yeye lakini inaonesha kuwa kwa sababu ikuwa Mnyama kabadilisha kocha na sisi pia hatushindwi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic