Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba ambaye kwa sasa ni mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe, amemvaa kipa namba moja wa timu hiyo, Aishi Manula kuwa alifanya uzembe katika mchezo dhidi ya Yanga.
Jumamosi iliyopita Yanga ilifanikiwa kutoka nyuma na kumaliza mechi dhidi ya Simba kwa sare ya mabao 2-2, mabao ambayo mashabiki wamekuwa wakimlaumu kipa namba moja wa timu hiyo Aishi Manula kuwa hakuwa kwenye ubora wake.
Akizungumza na kituo kimoja cha televisheni cha jijini Dar, Hans Poppe alisema kuwa, Manula amekuwa na upungufu katika suala zima la kudaka mabao ya mbali, huku akisema kuwa huenda mwalimu wake hampi mbinu za kutosha.
“Kuna upungufu kwa Manula au tekiniki anazofundishwa na kocha wake siyo nzuri, kwa sababu hata mtu ambaye hufahamu mpira unajua wazi kabisa mipira yote ya kona inayokuja ndani ya sita ni lazima kipa ushughulike nayo.
“Lakini wakati mwingine hafanyi hivyo, nafikiri mwalimu wake anatakiwa kulifanyia kazi hili,” alisema Hans Poppe.
Waooooooooh kaibuka tena kocha mkuu wa Simba,aliwahi kumsakama mmoja wa wachezaji waandamizi utafikiri yy kocha awezi kutoa maelezo ya ufundi hana historia ya madudu yanayofanywa na makipa bora dunia
ReplyDelete