Kocha mpya wa Klabu ya Yanga, Luc Eymael raia wa Ubelgiji tayari amewasili jijini Dar es Salaam na kuelekea Zanzibar jioni hii na ataungana na kikosi cha klabu hiyo hiyo kinachoshiriki Michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Eymael, ametua jijini Dar es Salaam leo Alhamisi, Januari 9, 2019, na ataanza kazi rasmi baada ya kumaliza taratibu za vibali vya kufanya kazi nchini. Leo Saa 2:15 usiku, Yanga itacheza mchezo wa nusu fainali dhidi ya Kombe la Mapinduzi na Timu ya Mtibwa.
Akizungumza mara baada ya kutua kwenye ardhi ya Bongo, Eymael amesema kuwa anaona fahari kujiunga na timu kubwa.
“Ni furaha yangu kuona kwamba nimepata timu kubwa ndani ya Afrika. Ninaitambua vema falsafa yake na namna ilivyo hivyo nina imani tutakwenda nayo sawa,” amesema Luc.
Kocha huyu ni viwango vya juu (FIFA, UEFA & CAF) matumaini yetu na ombi letu wadau wa soka na haswa mashabiki, wanachama, viongozi, benchi la ufundi na wachezaji wote wa Young Africans Sports Club wampe ushirikiano 101%
ReplyDeleteHakuna kocha hapo..takwimu zinaonyesha mgoogle na uingie wikipedia..kote alikoondoka nafasi zake ni 13, 14 na wakati league nyingi zina timu 16 hadi 18..
ReplyDelete