January 4, 2020


TANZANIA Prisons imeendelea kupata tabu kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kukubali kichapo cha pili kwenye ligi msimu huu mbele ya Coastal Union ya Tanga , Uwanja wa Mkwakwani.

Prisons ilicheza jumla ya mechi 12 bila kufungwa ilianza kupoteza mbele ya Yanga kwa kuchapwa bao 1-0 lililofungwa na Patrick Sibomana na jana imefungwa bao 1-0 mbele ya Coastal Union.

Kwenye mechi zake mbili mfululizo, Prisons iliyo chini ya Adolf Richard imekwama kupata hata pointi moja kutokana na kupokea kichapo.

 Kwa sasa ipo nafasi ya 10 baada ya kucheza mechi 14 ikiwa na pointi 20 kibindoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic