Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa haujaamua kumsajili kiungo aliyekuwa akiichezea Simba, James Kotei sababu hana ubora wa kuichezea timu hiyo.
Kwa mujibu wa Ofisa Uhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz, ameeleza kuwa Kotei kwa sasa hapewe nafasi ya kuichezea Yanga sababu tayari ina wachezaji wengine.
Amesema kuwa, Yanga imefanya usjajili mzuri kipindi hiki cha dirisha dogo na wala haina haja ya kuanza kupigania saini ya Kotei.
Kiungo huyo aliyefanya makubwa akiwa na Simba, hivi sasa anapiga soka lake kunako klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
0 COMMENTS:
Post a Comment