NAHODHA Msaidizi wa Yanga, Juma Abdul ambaye ni beki wa kulia amesema kuwa hawatishwi na wapinzani wao Simba kuelekea kwenye mchezo wao utakaopigwa leo. Januari, 4 uwanja wa Taifa bali wanawaheshimu.
Abdul mwenye asisti moja ndani ya ligi amecheza jumla ya mechi saba ambazo ni sawa na dakika 630 amekuwa kwenye ubora wake msimu huu baada ya kutoka kwenye majeraha msimu uliopita.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Abdul alisema kuwa maandalizi yapo vizuri na kila mchezaji amepewa majukumu yake ya kutimiza ili kufikia malengo ya kupata ushindi.
“Tumekuwa bora kwa sasa na kila siku kikosi na morali inaongezeka, kwa sasa hatuna mashaka na mchezo wetu dhidi ya Simba tutapambana kupata matokeo chanya kikubwa mashabiki watupe sapoti tunahitaji pointi tatu,” alisema.
Kwa upande wa Simba, beki kisiki Pascal Wawa ambaye amecheza jumla ya mechi tisa sawa na dakika 810 amesema kuwa hawana hofu na mchezo wao dhidi ya Yanga.
“Kama siku zote ambavyo huwa tunafanya kutazama mbele na kutafuta matokeo, kila mchezo ni muhimu kwetu kushinda, tunaamini katika Mungu na jitihada, mashabiki watupe sapoti,” alisema Wawa.
Simba iliyo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 34 baada ya kucheza mechi 13 itakuwa mwenyeii wa Yanga iliyo nafasi ya tano baada ya kucheza mechi 11 ikiwa na pointi 24 kibindoni.
0 COMMENTS:
Post a Comment