January 4, 2020


OLE Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa hamtambui mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Arsenal, Robin Van Persie ambaye alimchana kwa kitendo chake cha kuonyesha tabasamu licha ya kufungwa na Arsenal.
United ilichapwa mabao 2-0 na Arsenal kwenye mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Jumatano, Uwanja wa Emirates ila Solskkjaer alionekana kutabasamu wakati wa mahojiano na waandishi wa habari jambo ambalo Van Persie  aliponda suala hilo.
Van Persie alitoa maoni yake kwenye kipindi cha BT Sport baada ya kuona mahojiano ya Solkjaaer uwanja wa Emirates Jumatano usiku.
"Simjui Robin na Robin hanijui mimi, hana mamlaka na nguvu ya kunikebehi kwa namna anavyofikiria hiyo sio sawa namna yangu ya utawala na misimamo yangu haiwezi kubadilika," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic