Imefahamika kuwa Yanga imetumia kitita cha dola 15,000 (zaidi ya shilingi milioni 30) kufanikisha dili la usajili la mshambuliaji wa Gor Mahia ya Kenya, Muivory Coast, Yikpe Gnamien.
Yikpe alitua nchini hivi karibuni kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Yanga ili amwage wino wa kukipiga Jangwani kabla ya kufanyiwa vipimo na majaribio aliyofuzu na kupewa mkataba wa miaka miwili.
Muivory Coast huyo anakamilisha usajili huo na kufi kia idadi ya wachezaji watano waliosajiliwa kwenye dirisha dogo lililofunguliwa Desemba 16, mwaka jana kabla ya kufungwa Januari 15, 2020.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Yanga imefi kia hatua ya kutumia kitita hicho cha fedha kufanikisha dili hilo baada ya Kaimu.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Mkwasa kuvutiwa na kiwango chake akiwa kwenye majaribio. Mtoa taarifa huyo alisema kuwa awali hawakuwa na mipango ya kumsajili mshambuliaji huyo, lakini baada ya Mkwasa kuvutiwa naye fasta walimpa mkataba na kusaini.
Aliongeza kuwa mshambuliaji huyo atakuwepo kwenye sehemu ya kikosi cha timu hiyo kitakachoivaa Simba kwenye mchezo wa watani wa jadi utakaopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
“Tulitumia muda mrefu kidogo kufanikisha usajili wa Yikpe kwani licha ya kumuamini tulimpa muda kocha wetu Mkwasa wa kumuangalia mazoezini kabla ya kuruhusu kumsajili.
“Tunashukuru Matokeo viongozi kufanikisha usajili huo kwa haraka licha ya kumpa muda wa kumuangalia kwa lengo la kocha kujiridhisha na kiukweli walitakiwa kufanya hivyo kumpa muda wa kufanya mazoezi ili kuangaliwa kiwango chake kwa kuhofi a kile kilichotokea kwa akina Balinya (Juma).
“Baada ya kocha kuridhishwa na mshambuliaji huyo, haraka wakafanikisha usajili wake kwa dau la dola 15, 0000 akisaini mkataba wa miaka miwili ya kuichezea Yanga,” alisema mtoa taarifa huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment