Kiungo nyota wa zamani wa timu ya Yanga ambaye aliondoka kwa misimu miwili na kwenda kwa watani wao wa jadi, Simba SC, Haruna Niyonzima, raia wa Rwanda, hatimaye amerejea tena Yanga mapema leo Alhamisi, Januari 2, 2020.
Niyonzima ambaye aliichezea Yanga kwa miaka sita (2011-2017) alipoamua kujiunga na Simba alikodumu kwa miaka miwili (2017-2019) na kutimkia AS Kigali Rwanda, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na mashabiki wa Yanga wakiongozwa na mhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz, na wanahabari.
Niyonzima anarejea Yanga zikiwa zimesalia siku mbili kufikia Januari 4, ambapo watani wa jadi, Simba na Yanga, watavaana katika Dimba la Taifa.
“Ukitoka sehemu ukarudi ukiwa mzima, ni jambo la kumshukuru Mungu. Nipo hapa kwa ajili ya Yanga na si kitu kingine, jambo kubwa ni ushirikiano tu. Nakuja leo Tanzania kuungana na timu yangu (Yanga SC), kurejea nyumbani hiyo ni ishara kuwa nipo tayari kuwafanyia kazi, kwa hiyo kama kuna makosa yalitokea awali naomba tuyasahau.
“Naomba ushirikiano na upendo kama niliopewa kipindi nakuja kujiunga Yanga kwa mara ya kwanza. Nipo tayari hata kwa mchezo dhidi ya Simba SC japo sipendi kuongelea sana kwa maana mechi hizi zina mambo mengi sana lakini kikubwa ni kujiandaa kisaikolojia. Narudi nyumbani Yanga,” amesema
Hakuna cha ajabu mke mulimuwacha tukamuowa sisi na sisi tumemuacha mmemuowa tena nyinyi kandambili sasa cha ajabu nini zaidi ya ujinga kuliko ujinga subirini tarehe 4. Mtakula 4G
ReplyDeleteunaonekana wewe ni mbumbumbu na shabiki maandazi ktk soka!!!!!!,hata hujui kuwa haruna aliamua mwenyewe kuondoka simba baada ya mkataba wake kwisha na sio kuwa mlimuacha kama unavyofikiri.......waulize mashabiki wenzako wanaoujua mpira wa bongo na kuufuatilia watakufungua akili na mawazo yako mgando.
DeleteMkitaka kuua Simba kirahisi ni lazima muwatumie nyota wenu wapya wote kwa mkupuo moja
ReplyDeleteWatoto wa sheikh yahya utawajua tuu
ReplyDelete