January 16, 2020


Uongozi wa klabu ya Simba umeamua kumrejesha winga wake wa zamani Shiza Kichuya.

Mchezaji huyo alikuwa sehemu ya kikosi cha kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi hapo awali kabla ya kuelekea Misri kucheza soka la kulipwa.

Haijafahamika kipi kimemkuta Kichuya huko Misri lakini mabosi wake wa zamani wameamua kumrejesha kazini Msimbazi.

Inaelezwa kuwa Kichuya amesaini mkataba wa miaka miwili.

11 COMMENTS:

  1. kwahili tumefeli simba coz kocha sio pendekezo lake hili

    ReplyDelete
  2. Ameshindwa kucheza timu ndogo Misri then tunataka kufikia levels za kina AlAhly, Mazembe. Sijui mchawi wetu nani jamani.

    ReplyDelete
  3. Ujinga uliokithiri duh amakweli simba tumekua wazembe,kichuya wa kazi gani simba,ivi viongozi mpo kweli??na hata kama mpo mbona kama hampo makini?mmekabidhiwa majukumu kwakuzingatia weledi na ufanisi ambao tumedhani kwamba mnao,sasa iweje leo mnatuangusha?kwa hapa ilipokfika simba sio yakusajili aina hii ya wachezaji,mtu kashindwa kuonyesha kiwango kwenye timu ndogo huko leo atatusaidia nini?na pia haikua na ulazima wa kusajili nafasi hii kwani kuna mapungufu gani?acheni dhana za ajabu ajabu tumeshachoka ujinga wenu,kama bado kuna ukiritimba unaoendelea hapo simba tunaomba uishe maana ni dalili za wazi kabisa kwamba kuna watu wamekalia nafasi kwa ajili yakusaidia ndugu zao hata kama hatuna uhitaji nao,acheni ujinga plz.

    ReplyDelete
  4. Nyie hamjawaelewa viongozi wenu wa simba,wao wamefanya kuwafuatilia yanga kwa namna ambavyo walikuwa na nia ya kumsajili kichuya kwa kandarasi ya miezi 6,baada ya kusikia hivyo wao wakaona ngoja tuwakomoe yanga,ndio wakafikia kumpa kandarasi ya miaka2 lakin wala sio chaguo la bench la ufundi,mkijaribu kufuatilia hata huyo kiungo mshambuliaji wa UD SONG ambaye simba pia wamemsajilini kwa zilezile fikra za kuikomoa yanga kwa kujua kabisa yanga wanakaribia kumsajili wao wakaenda kumpa pia mkataba,ukiangalia pia hata issue ya JAMES KOTEI,Bado viongozi wa simba wako baadhi wakimhitaji kumrudisha lkn kuna wengine wanakataa,hilo ndio soka la bongo kuhisi kuwa unachukua mchezaji ambae huna plan nae lakin lengo kuu ni kumkomoa mpinzani wako

    ReplyDelete
  5. Kichuya na luis miqquisone ni type moja tumepoteza hela

    ReplyDelete
  6. Kicxhuya ni mchezaji talented na amekuzwa katika misingi ya soka.Simba kumrudisha kichuya si kosa kwani ni swala la kiufundi zaidi na ninyi ambao mnamziaki mpeni muda tu.kumbukaa mtu unapokwenda sehemu si lazima utapafom kwa kiasi kile wanachofikilia watu. je mnafatilia ligi ya misri kwa kiasi gani, je anapatiwa muda sahihi wa kucheza?/ wangapi wapo misri hapo na wanamuda mrefu tu na awana muendelezo mzuri na timu ya taifa wanaitwa kila mara.tumpe sapoti nahimani kubwa sana na huyu bwana mdogo.

    ReplyDelete
  7. Tunatowa wachezaji wazuri tunachukuwa wabovu

    ReplyDelete
  8. Mchawi alieturoga kafa. Hii yote ni kwa sababu ya poor scouting system. Mameneja wanapiga pesa kwa kueneza Yanga wanamtaka mchezaji X, kesho Simba wanakimbilia kusaini. Simba tumekuwa na ugonjwa mbovu. Pia mchezaji akiifunga Simba ajue next season anasajiliwa. Huyu wa UD Songo nae mweupe kabisa sijui tumepoteza pesa za nini. Leo gazeti likiandika Yanga wanamtaka Mwameja arudi kuwadakia, kesho utasikia Simba wamemkimbilia mwameja nyumbani na kumsainisha. Tunacheza ngoma inayopigwa na watengeneza pesa kuuza wachezaji wao. Yule Kibaya au Nchimbi ni wazuri kuliko huyo Kichuya.

    ReplyDelete
  9. Halafu badae timu ikifanya vibaya lawama kwa kocha unataka kufikia leval ya tp mazembe kwa siasa kama hizo thubutu

    ReplyDelete
  10. KUNA MWENYE SWALI KUHUSIANA NA KAMATI YA USAJILI YA SIMBA?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic