January 19, 2020


KOCHA wa Tottenham Hotspur, Jose Mourinho, amesema kuwa kiungo wake, Christian Eriksen aondoke akiwa nafuraha. Mara kwa mara kiungo huyo amekuwa akitajwa kuwa anataka kuondoka kwenye timu hiyo kwenye usajili huu wa Januari.

Hata hivyo, juzi alionekana kuwaaga wachezaji na mashabiki wa timu hiyo wakati Spurs ilipokuwa ikivaana na Middlesbrough kwenye mchezo wa Kombe la FA. Eriksen aliwaaga mashabiki wa timu hiyo kwa kuwa pungia mkono na kumpa shabiki jezi yake aliyotumia kwenye mchezo huo.

“Nafikiri anatakiwa kuondoka hapa akiwa na furaha ni mchezaji mkubwa na amekuwa akionyesha kiwango cha juu sana kwenye kila mchezo.

“Hakika amekuwa mtii sana kwenye timu hii, ameonyesha uanamichezo kwa muda wote ambao yupo hapa, nafikiri anatakiwa kuondoka akiwa amenyanyua kichwa chake juu,” alisema Mourinho.

Staa huyo ambaye ni raia wa Denmark anatarajiwa kuondoka kwenye timu hiyo na kujiunga na Inter Milan.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic