January 19, 2020


Kocha wa Yanga, Luc Eymael amewacharukiwa wachezaji wa kikosi hicho baada ya kushindwa kutumia nafasi walizotengeneza kupata mabao ya haraka ambayo yangewatoa mchezoni wapinzani wao.

Eymael ametoa kauli hiyo baada ya kocha huyo kuanza vibaya kibarua chake kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Eymael alisema kikosi chake kipindi fulani walionekana kuzidiwa sehemu ya kiungo na wapinzani na kuwapa mwaya wa kufunga lakini walitengeneza nafasi nyingi kwenye eneo la hatari ambazo nyota wake walishindwa kutumia.

“Mchezo ulikuwa mgumu kwani wapinzani wetu walicheza kwa kujiamini na kumiliki sehemu ya kiungo pamoja na hivyo kwa kiasi fulani na tulikuwa wazuri kwa kutengeneza nafasi nyingi ambazo zilishindwa kutumika ipasavyo,” alisema Eymael.

Alisema kipindi cha pili wachezaji wake walionekana kurudia kufanya makosa yaliyowagharimu kipindi cha kwanza licha ya kupewa maelekezo na kujikuta wakiwaacha tena wapinzani kuchezea mpira kwa uhuru na kufunga tena mabao mawili.



3 COMMENTS:

  1. Hofu yangu ni kuwa MASHABIKI WENYE HASIRA WA YANGA MSIANZISHE KAMPENI KUDHURU MAREFA KWANI AMANI ITAONDOKA VIWANJA VYA SOKA. OMBI BODI YA LIGI NA TFF WAAMBIENI WAAMUZI WACHEZESHE KWA HAKI KWANI LA SIVYO UMEWASIKIA MASHABIKI WA YANGA NA MIKAKATI YAO!

    ReplyDelete
  2. Manaake Yanga wanamtaka lazima washinde kwakuwa wametumia hela nyingi za usajili sio kuwa timu ina kiwango. Yanga ina papara za kusajili ili wahakikishe wanamnyanganya Mnyama alietulia ubingwa na ndio wanazidi kujivuruga na huku GSM wakitarajia makubwa kwa jinsi walivojizatiti kwa hali na Mali lakini hakuna cha kuwapa moyo

    ReplyDelete
  3. Ligi bado Sana, kwenye soka lolote kinaweza tokea.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic