STRAIKA mpya wa Yanga, Tariq Seif, yupo fiti baada ya kupona majeraha ya nyama za paja yaliyomfanya akae nje kwa siku kadhaa.
Tariq aliyejiunga na Yanga katika usajili wa dirisha dogo, alipata majeraha hayo katika mchezo wa Ligi Kuu Bara msimu huu dhidi ya Biashara United ambapo alifunga bao katika ushindi wa 1-0.
Daktari wa Yanga, Sheck Mngazija, alisema: “Tariq tayari ameshakuwa sawa baada ya kufanyiwa matibabu.
“Baada ya kupona kwake, hivi sasa hakuna majeruhi yeyote kwa timu yetu, hivyo wachezaji wote wa Yanga wapo fi ti kwa ajili ya kucheza.”
Timu ya kuuzia magazeti. Wapuuzi wanapelekwa puta na makanjanja wao.
ReplyDelete