January 9, 2020


Wakati mashabiki wa soka hapa nchini wakiendelea kupishana kauli juu ya mshambuliaji wa Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere kuwa alikuwa na hirizi uwanjani katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga huku wengine wakipinga, Championi Jumatano limepata ukweli wa jambo hilo.

Simba na Yanga zilicheza Jumamosi iliyopita kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2 kwenye Uwanja wa Taifa.

Katika mitaa mbalimbali hapa nchini jambo hilo limekuwa gumzo kubwa lakini kila mtu amekuwa akisema la kwake bila ya kuwa na ukweli wowote.

Hata hivyo, kutokana na hali hiyo mmoja wa waamuzi waliochezesha mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa, ameliambia gazeti hili kuwa, Kagere hakuwa na hirizi katika mchezo huo kama wengi wanavyofikiria.

“Watu wengi tumetawaliwa sana na mawazo ya ajabu na yasiyokuwa na faida yoyote katika maendeleo ya soka letu.

“Kagere hakuwa na hirizi katika mchezo huo bali ile ilikuwa ni cheni ambayo aliokota uwanjani na kumpatia mwamuzi Jonesia Rukyaa ambaye pia aliipeleka kwa mwamuzi wa akiba naye akaipeleka katika benchi la ufundi la Simba.

“Kwa hiyo, hao wanaosema kuwa Kagere alikuwa na hirizi katika mchezo huo ni waongo, niwaombe tu wasiwe wepesi wa kusema vitu wasivyokuwa na uhakika navyo, hata kama utamuuliza Rukyaa naye atakwambia hivyo hivyo, japokuwa maadili hayaturuhusu kusema chochote kabla ripoti zetu kufanyiwa kazi na TFF,” alisema mwamuzi huyo kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini.

CHANZO: CHAMPIONI

11 COMMENTS:

  1. Ndugu mwandishi mtaje mwamuzi yupi huyo,ili tumuulize na sisi Cheni gani hiyo yenye kitambaa cheusi,na kama ni Cheni na yeye ni mchezaji mkubwa kwa nini hakuivua ilhali anajua kisheria huwezi ingia uwanjani na vito, ni naona kwa mwonekano wake tu kagere siwezi kuamini ile et ilikuwa cheni

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amesema kagere aliikota uwanjani na kumptia muamuzi...sa atavaaje na mali sio yake kaka

      Delete
    2. Miwatu ya yanga uelewa wao ni mzito sana

      Delete
  2. Abdalah rudia kutizama kipande cha video wakati yule mama refa anaenda kupelekea kwa refa wa akiba pale nje nae anamrushia kwa matola uone kama ni hirizi sema mashabiki tumekuwa tunazusha mambo sana

    ReplyDelete
  3. Toeni hoja sio mapovu! Hivi Kagere aliokota na kumpa refa au alishinikizwa na Yondani? Ni cheni gani inavishwa kitambaa cheusi? Au mnazungumzia tukio jingine zaidi ya LA mechi ya mtani?

    ReplyDelete
  4. KAMA ALIIOKOTA UWANJANI ILIKUAJE IPELEKWE KWENYE BENCHI LA UFUNDI LA SIMBA????!!!! MAANA MWENYE NAYO HAJULIKANI. KWANZA KWA UTARATIBU ILITAKIWA KUBAKIA KWA KAMISAA WA MCHEZO ILI AIAMBATANISHE KWENYE RIPOTI YA MCHEZO. MAANA NI KITU AMBACHO HAKIKUA SEHEMU YA MCHEZO KWA HIYO KILIPASWA KURIPOTIWA NA KUAMBATANISHWA KAMA USHAHIDI. KWA MKANGANYIKO HUO LAZIMA TUBAKIWE NA MASWALI MENGI.

    ReplyDelete
  5. Simba michawiiiiiii na washirikina

    ReplyDelete
  6. Wewe mwandishi tunakujua kua wewe ni simba,unatumia taaluma yako kuitetea simba kwa upuuzi alioufanya kagere,ile ni hirizi na tumeiona waziwazi ikiwa na rangi nyeusi,achakudanganya watu.

    ReplyDelete
  7. Yanga wabishi sana.....kama hujui kuwa refa anashika filimbi..so mkono wake ulishika filimbi na cheni...kutokana na hofu yenu kwa kagere mkadhani filimbi ndio hiriz ya kagere....noma sana....mshukuru matokeo yalikuwa upande wenu....mngepoteana.

    ReplyDelete
  8. Maelezo ya kagere nikua ni cheni yake ya dhahabu alisahau kuivua wakati wanatoka kupasha misuli kabla ya mechi mwandishi Fara anadai kagere kaokota uwanjani jaman waandishi wengine vilaza amesahau juzi ameandika tofauti tena blog hihii sasa kwani cheni haiwezi kutumika Kwa imani za kishirikina???waamuzi hawakumkagua hadi anakaguliwa na wachezaji uwanjani???na kwann aifiche kwapani???tusipende kutetea ujinga kwenye ligi yetu kwan ndo maendeleo ya mpira nchini

    ReplyDelete
  9. We una uhakika gani kama ni hirizi na sio cheni mana yake ata wewe ni mchawi uwezi kuwa na mawazo ya kishirikina kama wewe si mshirikina Kagere kaokota cheni kwenye boksi lenu la kumi nane leo hii mnamsingizia kaingia na hirizi kama mnaamini katika hirizi basi zitumieni ata nyinyi zinaweza kuwasaidia wachawi wakubwa msiojua nini mpira, Kelele kibao nje ya uwanjwa lakini siku mksikia mnacheza na Simba Chupi zinawabana uwanjani kuja mnaogopa alafu nnje ya uwanja nyie ndo mnaaongoza kuongea ndo mana mi naamini ule msemo unaosema mtu akikwambia akili zako kama mshabiki wa Yanga pigana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic