January 8, 2020



NAHODHA wa Lipuli, Paul Nonga amesema kuwa malengo makubwa ya timu yao ni kuwa ndani ya tano bora jambo linalowafanya wapambane muda wote.

Nonga ni kinara wa utupiaji kwa wachezaji wazawa akiwa nayo nane na ana jumla ya pasi nne za mabao.

"Tunatambua tuna kazi kubwa ya kufanya kwenye ligi pamoja na mashindano mengine kikubwa kinachotupa mafanikio ni juhudi za kila mchezaji kutafuta matokeo chanya," amesema.

Lipuli leo itakuwa uwanja wa Uhuru kumenyana na KMC kwenye mchezo wa ligi ipo nafasi ya tano na pointi zake 24 huku KMC ikiwa nafasi ya 17 na pointi zake 13 na zote zimecheza mechi 15.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic