January 8, 2020


Inaelezwa bao la kusawazisha la kiungo wa Yanga, Mohammed Issa ‘Mo Banka’, limepelekea kifo cha shabiki wa timu hiyo sajenti Omari Minguya wa Jeshi la Magereza Kitengo cha Redio jijini Dar.

Askari huyo ambaye inadaiwa kuwa ni shabiki kindakindaki wa Yanga, alipatwa na umauti huo baada ya timu yake kupata bao la kusawazisha katika mchezo uliopigwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa. Mchezo ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Taarifa zinadai kuwa rafiki yao alipatwa na mshtuko juzi jioni wakati alipokuwa akifuatulia matangazo ya mchezo wa Simba na Yanga kwenye runinga nyumbani kwake Ukonga jijini kabla ya kupatwa na umauti baada ya kukimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Championi Jumatatu lilimtafuta Msemaji wa Jeshi la Magereza, SSP, Amina Kavirondo alisema wamepokea kifo cha sajenti huyo ambapo wametuma maofisa wa jeshi hilo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kifo kabla ya leo Jumatatu kutoa taarifa kamili ya kifo hicho.

“Kiukweli tumepokea kwa masikitiko kifo cha askari wetu lakini hatuwezi kusema nini kimepelekea kifo chake kwa sasa kwa sababu tumewatuma wataalam wetu kwenda kufanya uchunguzi na kesho (juzu) Jumatatu mapema tutatoa taarifa kamili,” alisema Kavirondo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic