January 3, 2020


BAADA ya kukamilisha usajili na utambulisho wa kiungo aliyekuwa anakipiga ndani ya UD Songo, Luis Miquissone leo amejiunga na kikosi cha Simba kufanya mazoezi ya mwisho.

Simba imemtambulisha nyota huyo ambaye alikuwa amewekwa kwenye hesabu za Yanga kwenye dirisha dogo akiwa ni mchezaji wao wa kwanza kusajiliwa.

Kwenye mazoezi ya mwisho ya leo yaliyofanyika viwanja vya Mo Simba Arena, Luis alikuwa ndani ya uwanja akifanya mazoezi na wachezaji wa Simba watakaoshuka kesho kumenyana na Yanga uwanja wa Taifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic