January 9, 2020


Waziri Mkuu mpya wa Finland Sanna Marin amependekeza nchi hiyo iwe na siku nne tu za kufanya kazi ambazo ni sawa na saa 96 ili wananchi wawe na fursa kuwa na familia zao kwa muda mrefu Zaidi na kufanya mambo mengine ya jamii ikiwemo michezo na utamaduni.

Marin, akiwa kiongozi mkuu wa serikali mdogo kuliko wote duniani kwa kuongoza nchi hiyo akiwa na umri wa miaka 34, amependekeza pia kwamba muda wa kazi uwe saa sita badala ya nane kwa siku.

Kiongozi huyo mwenye mtoto mmoja anaongoza muungano wa vyama vya mlengo wa kati-na-kushoto akiwa na viongozi wengine wa vyama vinne ambavyo vitatu vinaongozwa na wadada wenye umri wa chini ya miaka 35.

Katika mahojiano alisema: “Naamini wananchi wana haki ya kutumia muda wao mwingi na familia zao, wapenzi wao na mambo mengine katika Maisha kama vile hobby na utamaduni. Hii itakuwa hatua kubwa kwetu katika Maisha ya kazi”.

Kabla ya kuwa Waziri Mkuu Marin alikuwa Waziri wa Uchukuzi wa Finland, ambapo hata huko wizarani alipigania suala la kuwa na siku chache za kufanya kazi katika wiki ili kuongeza ufanisi na tija.

Hivi sasa nchini Finland kufanya kazi saa nane kwa siku na siku tano kwa wiki ni jambo la kawaida. Pendekezo hilo limeungwa mkono mara moja na Waziri wa Elimu wa nchi hiyo Bi. Li Andersson, ambaye ni kiongozi wa chama cha Left Alliance.


Bi. Andersson alisema: “Ni jambo la mihumu kuruhusu raia wa Ufini kufanya kazi kwa kiasi. Hili sio swala la kutawala kwa staili ya kijinsia bali pia ni kusaidia na kutekeleza ahadi kwa wapiga kura”.

Katika nchi jirani ya Sweden, ambako mfumo wa kufanya kazi kwa siku sita kwa wiki ulijaribiwa mwaka 2015, matokeo yalionesha kwamba wafanyakazi wamekuwa wenye furaha Zaidi, matajiri na wenye kuleta tija.

Mapema mwezi Desemba mwaka jana baraza la chama tawala cha nchio hiyo Social Democratic Party kilipitisha kwa kura 32-29 jina la Sanna Marin dhidi ya Antti Lindtman kuchukua kiti cha uwaziri mkuu kutoka kwa aliyekuwa anashika nafasi hiyo Antti Rinne.

Na mnamo Mwezi November mwaka jana kampuni ya Microsoft Japan ilifanya uamuzi mgumu wa kuboresha Maisha ya kazi kwa kuanzisha weekend ya siku tatu kwa wafanyakazi wake. Matokeo yalionesha tija kupanda kwa asilimia 39.9!

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic