SADIO Mane, nyota wa timu ya Taifa ya Senegal na timu ya Liverpool inayoshiriki Ligi Kuu England ametwaa tuzo ya mchezaji Bora wa mwaka 2019 kwa wachezaji wa Afrika. Jana kwenye usiku wa tuzo hizo .
Mane mwenye umri wa miaka 27 ameshinda tuzo yake hiyo kwa mara ya kwanza akichukua tuzo hiyo mikononi mwa mchezaji mwenzake wa Liverpool, Mohamed Salah raia wa Misri aliyetwaa tuzo hiyo mara tatu katika miaka ya 2017,2018 na 2016.
Mane anakuwa msenegali wa pili kutwaa tuzo hiyo baada ya mtu wa kwanza kuwa El Hadji Diof aliyetwaa tuzo hiyo mwaka 2001 na 2002.
0 COMMENTS:
Post a Comment