January 16, 2020


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye ni shabiki kindakindaki wa klabu ya Simba, amehoji juu ya matumizi ya Sh. bilioni 4 alizotumia mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji 'Mo' kulipa mishahara.

Hiyo imekuja kufuatia mwekezaji huyo kuamua kujiuzulu nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, muda mfupi baada ya Simba kufungwa na Mtibwa Sugar katika fainali ya Mapinduzi Cup visiwani Zanzibar, Januari 13 2020.

Dkt. Kingwangalla ambaye aniwakilisha serikali katika wizara hiyo ya Utalii, amehoji kuwa hizo bilioni nne ambazo Mo amelipa kama mishahara ndani ya klabu hiyo zimefanyika kwa makubaliano gani na kwa kujiondoa kwake katika nafasi hiyo, mishahara itaendelea kulipwaje?

"Poleni wanasimba wenzangu, ‘kisukari kimetuvuruga’, hivi kuna mtu anaweza kunisaidia? Hii mishahara ya 4bn iliyolipwa na Mo inalipwa kwa makubaliano gani? Isijekuwa ndiyo katika ile 20bn ya manunuzi ya hisa 50%, ama manunuzi yalikwishafanyika? Anavyojitoa, italipwaje?

Baada ya mchezo wa fainali ya Mapinduzi Cup kumalizika kwa Simba kupoteza kwa bao moja mbele ya Mtibwa Sugar, bilionea Mo Dewji akaandika katika ukurasa wake wa Twitter ujumbe kuwa hatoendelea na nafasi yake, atabakia kama mwekezaji na nguvu kubwa ataiwekeza kwenye miundombinu na soka la vijana.

3 COMMENTS:

  1. Sasa andiko la Kigwangala ndio limekuwa andiko la serikali? Nembo ya serikali au muhuri wa serikali uko wapi kwenye hilo andiko? Na watu wenye dhamana zao kwanini wanaachia huu upumbavu wa kulishiwa maneno serikali uendelee? Kigwangala ni mtu mwenye muwasho wa aina yake kwenye account yake ya Twitter.Mara nyingi huvurumisha mawazo yake binafsi hata kwa watumishi wenzanke wa ngazi za juu bila kufuata taratibu za kiongozi. Na baada ya Mo kutangaza kujiuzulu Kigwangala alidhamiria kuona Simba inaingia kwenye malumbano na migogoro zaidi.Na ndipo Makonda alipoonyesha ukomavu wa kisiasa.Na ndipo siku zote Nasema Makufuli si mpumbavu kumkabidhi Makonda kuongoza jiiji tata kama Daresalam. Hii taharuki ya Simba imeonesha Makonda ni nani katika kudumisha amani ndani ya jamii ya watanzania.

    ReplyDelete
  2. Ni transition period tunapitia gari halijaa kaa sawa yaani unamchukia Diamond halafu unaipenda #BABA_LAOπŸ˜›πŸ˜›πŸ˜›

    ReplyDelete
  3. DAH,HII SINEMA NI KALI SANA NATAMANI KUJUA MWISHO WAKE

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic