Baada ya kuibuka na ushindi wa penati 3-2 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa nusu fainali ya Mapinduzi CUP, baadhi ya mashabiki wa Simba wamemtupia lawama kipa Razak Abalora.
Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa penati hizo kufuatia dakika 90 kumalizika kwa suluhu ya 0-0.
Mashabiki hao wameeleza kuwa Abalora alikuwa akipoteza muda hovyo ili kuifanya mechi imalizike kwa suluhu wakisema alikuwa akijiamini kucheza matuta.
Wameeleza kuwa ni kipa mzuri lakini amekuwa na hali ya kujiamini sana kiasi cha kwamba akakosa penati ya mwisho kwa Azam ambayo ilichezwa na kipa Beno Kakolanya iliyoifanya Simba kutinga fainali.
Kwa sasa Simba itakutana na Mtibwa Sugar iliyotinga fainali kwa kuiondoa Yanga ambayo hivi sasa isharejea jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment