Klabu ya soka ya Simba imethibitisha kuwa uwanja wao wa Mo Simba Arena, uliopo Bunju utaanza kutumika kwenye michuano ya ligi kuu ya soka ya wanawake Tanzania Bara.
Katika mchezo uliopita wa ligi hiyo, Simba ilianza kibarua cha kucheza dhidi ya Kigoma Sisters ambayo ilimalizika kwa sare ya 1-1.
Kabla ya mchezo, Simba walitoa taarifa kupitia ukurasa wao wa Instagram kwa kuandika:,
'Timu ya Simba Queens leo inacheza mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake dhidi ya Kigoma Sisters. Mchezo huo unapigwa kwenye uwanja wa Mo Simba Arena kuanzia saa 10:00 jioni', imeeleza taarifa hiyo.
Uwanja wa Mo Simba Arena wenye viwanja viwili ambavyo pia vinatumika na timu ya wanaume ya Simba kufanyia mazoezi, ulipokelewa na klabu pamoja na mashabiki kutoka kwa mkandarasi Desemba 7, 2019.
e fggtr j
ReplyDeleteNa jangwani panatumika mashindano ya vyura na kambare yanaanza wiki ijayo jamani
ReplyDelete