Kuelekea pambano la watani wa jadi Simba na Yanga linalotarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewaonya mashabiki wa timu hizo kwa kuwataka kuwa wastaarabu wakati wote wa mchezo huo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa, alisema wamejipanga kikamilifu kuimarisha ulinzi katika mchezo huo, akiwataka mashabiki wote watakaofika kutazama mchezo huyo kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani.
Alisema pamoja na mapenzi yao kwa timu hizo, mashabiki hao wanatakiwa kushabikia mchezo huo kwa ustaraabu bila kurushiana chupa na kuharibu miundombinu ya uwanja na mambo mengine jambo litakaoufanya mchezo huo kumalizika kwa amani.
“Hatutasita kuwachukulia hatua kali watu wote watakaofanya mambo yasiyo ya kistaarabu siku ya mchezo huo, tutakuwa tumejipanga na kujiimarisha katika maeneo yote ya uwanja ili kuhakikisha mchezo unamalizika bila kuwapo na vurugu kutoka kwa mashabiki,” alisema Mambosasa.
Mfumo wa Uendeshaji wa Klabu ya Simba ni wa kisasa zaidi na unafaa kuigwa....kuiendesha klabu kubwa kama Yanga kwa staili ya ufadhili ni karne ya 19....ukiwa unaendesha kwa mfumo wa hisa na uwekezaji klabu inakuwa kampuni inaajiri watu wa kufanya kazi kuiendesha kama kampuni na mipango yake inakuwa ya kisasa (wataalamu wa soka/walimu waliobobea, wataalamu wa fitness, Lishe ya wachezaji, Wachua misuli, afya za wachezaji, match analysts, kambi bora na ratiba bora ya mazoezi, viwanja vya kisasa vya mazoezi na academy za soka kwa vijana) ..sio mwanachama huyu anateuliwa kwenye kamati hii au Ile, wachezaji mishahara inachelewa baadaye wanagoma, matibabu ya wachezaji kuchukua mwaka, ni baadhi ya changamoto za kuiendesha klabu kizamani kama Yanga
ReplyDeleteUmeongea points sana mwana yanga wanatakiwa kubadilika
DeleteKwa habari motomoto za michezo na burudani tutembelee katika Blog yetu https://www.jacoteltv.com
Waambie hao wana jangwani mambo yamebadilika
ReplyDelete