FRANCIS Kahata, kiungo wa Simba leo amewainua mashabiki wa Simba kwa kufunga bao la ushindi lililowapeleka hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho mbele ya Mwadui FC, Uwanja wa Taifa wakati Simba ikishinda mabao 2-1.
Mchezo wa leo ulikuwa ni wa kisasi kwa Simba baada ya kuchapwa bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara na bao lilifungwa na Mdamu ambaye leo amefunga pia bao kwa Mwadui. Mwadui FC ilianza kufunga bao la kwanza dakika ya 34 kupitia kwa Gerald Mdamu dakika ya 34 akimalizia pasi ya Ludovick.
Bao pekee la kuweka mzani kwa Simba lilifungwa na Clatous Chama akiwa nje ya 18 dakika ya 45+2.
Kipindi cha pili Simba walifanya mashambulizi ya kutafuta bao la ushindi sawa na Mwadui na dakika ya 84 ilijiandikia bao la pili la ushindi kupitia kwa Francis Kahata aliyemalizia pasi ya Shomari Kapombe kwa kichwa na kuwanyanyua mashabiki wa Simba.
Simba inatinga hatua ya 16 ya kombe la Shirikisho na Mwadui FC inafungasha virago jumla.
kwanza naipongeza timu yangu ya simba kutinga 16 bora kombe la ASFC 2019/2020. Hata hivo kuna tatizo la uchoyo miongoni mwa wachezaji wetu. benchi la ufundi tafadhali ttueni changamoto hii
ReplyDeleteMfumo wa kocha utamuondoa kagere kwenye kikosi,kagere ameshindwa kabisa kuonyesha kile kiwango chake na tusipoangalia simba haitasonga mbele kwenye asfc na huku kwenye ligi kuu nako simba akifanya mchezo anapoteza ubingwa,ukifanya tathmin inaonekana wazi dhahiri shahiri kikosi cha leo kilicho cheza na mwadui mwalimu hakukiandaa kabisa ndiomana akina ajibu mkude na dilunga na kagere walikua wanachanganyana sana,kama wanekua wamefanya maandalizi pangekua kuna combination maalumu na wala tusingeshuhudia vile vituko tulivyoviona leo,kwa mpira huu wala simba isitarajie ubingwa kamwe.
ReplyDeleteHawa wa matopeni haweshi porojo. Mnyama Kashinda yeye anasema asitaraji ubingwa. Pole baba
ReplyDeleteShis is simba
ReplyDeleteKwa povu hilo peleka maombi uwe kocha wa Simba .Tatizo la makocha wa keyboard ndio hilo .Kila mtu mjuaji .Leo kafungwa Barcelona 2 -0 na Valencia baada ya miaka 13 ya vipigo .Mpira ndio ulivyo judgement za kijinga za kuamua matokeo ya timu kwa mechi moja tena iliyoshinda ni upuuzi mtupu.
ReplyDeleteWachezaji waache uvivu na wajitume kwa kucheza kwa nguvu.
ReplyDeleteMwadui kafungwa goli moja na Azam kwa shida sana.Halafu anakuja zezeta wa akili analalamikia ushindi wa Simba. Huyu kocha ni kiboko labda tumpongeze Matola vile vile kwani mechi kama hii mbele ya kocha kama Aussems au mzee wa Uchebe,Simba wasingekuwa na mbinu nyengine tena ya kulirejesha lile bao, wangefungwa tu. Mwadui wameingia uwanjani na mbinu ile ile iliyowawezesha kuifunga Simba kwenye ligi kuu ila kwa upande wa benchi la ufundi la Simba kubadilika ndiko kulikoiokoa Simba leo,Hongera sana Simba.Simba kufunga magoli kwa kuwatumia viungo ndio suluhisho pekee la kushinda mechi zao kwani timu nyingi zinaingia uwanjani zikiwa tayari na mbinu za kumzibiti kagere asifunge.Hata hivyo Simba kuna kajiuzembe fulani unaendelea klabuni pale kwani kwa siku nyingi Simba inahitaji mshambuliaji wa uhakika wa kusaidiana na kagere pale mbele. Boko siku nyingi hayuko vizuri .Ni fowadi mzuri kweli lakini anakosa umakini pale mbele kutumia nafasi zinazotengenezwa na timu. Ila vijana wetu pia kama Dilunga bado wamelala usingizi. Hasa Dilunga kama angekuwa makini katika kufunga basi Simba ingesahau Suala la kutafuta mshambuliaji. Dilunga ana kasi,ana mashuti makali tatizo anakosa utulivu. Lazima kutakuwa kuna kitu anashiriki kinachomuondelea umakini mchezoni. Ila akijitafakari kidogo tu basi Hassan Dilunga ndie Sadio Mane wa Bongo no doubt about it. John Boko kwa kocha huyu aisipokuwa makini nae basi safari ya kuondoka simba kwa Boko inanukia.Timu nyingi zikicheza na Simba zinakamia kupita maelezo na sio jambo la kushangaza kwani mti wenye matunda ndio wenye kupigwa mawe. Usisahau pia Simba ndio malango alietokea Samata hapa bongo kwenda nje kila mchezaji angetamani kupitia mlango ule ule aliepitia samata nadhani. Hivyo mechi yeyote ya simba kwa timu nyingi za ligi kuu ni zaidi ya fainali isipokuwa wachezaji wa Simba wao huchukulia poa na matokeo yake wanajikuta wapo katika wakati mgumu ila benchi hili la ufundi la sasa la Simba kwa kweli kwa kipindi kifupi wameonesha utofauti mkubwa katika masuala ya kimbinu hasa pale timu inapokuwa chini kimatokeo,hongereni sana Simba.
ReplyDeleteVyura vinatamaa Sana kuvhukuwa ubingw Masikini Roho zao
ReplyDelete