January 2, 2020


UONGOZI wa Singida United umesema kuwa utaongeza wachezaji wakongwe ndani ya timu hiyo ili kuongeza nguvu ndani ya Ligi Kuu Bara.

Singida United imekamilisha usajili wa Athuman Idd Chuji nyota wa zamani wa timu ya Simba na Yanga kwenye dirisha dogo la usajili alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Azam FC.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa mpango mkubwa wa Singida United ni kupata matokeo chanya na kufanya usajili makini.

"Kuna mengi ambayo tunapitia kwa sasa ila kikubwa ambacho tunakifanya ni kuongeza wachezaji wenye uzoefu kwa ajili ya kuleta ushindani," amesema.

Singida United ipo nafasi ya 20 ikiwa na pointi saba baada ya kucheza mechi 14 za ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic