January 16, 2020


Inaelezwa kuwa kuwa kiungo wa Yanga, Mkongomani, Papy Tshishimbi ametimkia  kwao Congo kuangalia familia yake.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Luc Eymael, alisema Papy alimuaga siku moja kabla ya kuanza nao mazoezi, kuwa anamatatizo ya kifamilia hivyo  anasafiri kwenda kuwaona jamaa zake.

Hata hivyo alisema amempa siku chache kwa kuwa hajawahi kuwa pamoja nae mazoezini tangu ameanza, hivyo anatakiwa kuwahi ili apate muda wa kumsoma vizuri.

“Nimefuatilia baadhi ya video za Yanga, Papy ni mchezaji mzuri, lakini nahitaji awahi kurudi ili afanye mazoezi na wenzake kwani  tunakazi kubwa  ambayo inatukabili mbele yetu,”alisema Eymael.

Taarifa inasema kuwa, hata hivyo Tshishimbi ameeleza kuwa familia yake kwa sasa ipo salama, hivyo anatarajia kurudi kabbla ya mchezo wao dhidi ya Azam FC.

“Sikupanga kuja nyumbani kwa  kipindi hiki lakini amenilazimu kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezon wangu, lakini nitarudi haraka  sitaki kukosa mechi ya Azam, pia sijahudhuria maoezi na kocha wetu mpya tangu ameanza,”alisema Tshishimbi.

3 COMMENTS:

  1. Kwanini aondoke kipindi hiki cha mechi ngumu kumbuka banka ana red,shishimbi hayupo kweli azam atatuacha jamani tunazidi kumpa gape mnyama alafu tukiitwa wa madimbwini tunakasirika,yanga hili haliko sawa jamani jaribuni kuliangalia kwa jicho la tofauti runaomba.

    ReplyDelete
  2. Kwa mara ya kwanza kwa nchi kama Tanzania wachezaji wakitaka kuondoka matatizo ya kifamilia wanaenda lakini wenzetu. Mchezaji huwezi kuwasiliana na familia moja kwa moja na ndo maana hata mchezaji akifiwa mzazi anakichafua kwanza uwanjani baadae ndo anaambiwa kuna hili lakini sisi hata keshi kuna mechi ya muhimu mchezaji anaondoka leo hili haliko sawa na viongozi wanatakiwa waliangalie hao ni waajiriwa kama waajiriwa wengne tu.

    ReplyDelete
  3. Uandishi mbovu wa kishamba unatengeneza taharuki unnecessarily. Sijui kwa nini huu mtandao haubadiliki. Mbona mnaweza publish news zenu za michezo professionally na mkafanya business kwa kuheshimika.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic