January 17, 2020


UONGOZI wa Mbao FC umefanikiwa kusajili wachezaji sita katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo lililofungwa juzi usiku.

Akizungumza jana, Mwenyekiti wa timu hiyo, Solly Njashi alisema wamejipanga kuhakikisha timu yao inafanya vyema katika michezo ya ligi kuu iliyobakia.

Aliwataja waliosajiliwa ni Hussein Iddi kutoka Mtibwa Sugar, Omary Wayne kutoka Friends Rangers, Wilson Wilson, wote wamesaini mkataba wa miaka miwili.

Wengine ni Mackyada Franco kutoka Coastal Union kwa mkataba wa miezi sita, Hamis Mwinshehe kutoka JKU ya Zanzibar kwa mkataba wa mwaka mmoja na Paul Maige kutoka timu ya vijana ya Azam FC ya vijana chini ya miaka 20 kwa mkataba wa miaka mitatu.

Kocha mkuu wa timu hiyo, Hemed Morocco amesema ana imani na wachezaji kwani watasaidia timu yao iweze kufanya vyema katika michezo ya ligi kuu.

Alisema anawaomba wadau na wapenzi wa soka mkoani Mwanza wahakikishe wanajitokeza kwa wingi kuisapoti timu katika michezo yao yote ya ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic