Yanga imeajiri kocha mwingine ajulikanaye kwa
jina la Riedoh Berdien, raia wa Afrika Kusini.
Berdien atakuwa msaidizi wa Luc Eymael na kazi
yake kubwa ni fiziki ya miili ya wachezaji. Na taarifa zimeeleza atakaa kwa muda kuhakikisha kikosi kinakuwa na fiziki ya kutosha.
Kabla ya kukubaliana na Yanga, Berdien amewahi
kufanya kazi sehemu mbalimbali ikiwemo nchini Afrika Kusini katika klabu za Chippa
United na Free State.
Pamoja na hivyo, Berdien amekuwa chini ya
makocha wawili tofauti waliowahi kuifundisha Yanga.
Aliwahi kufanya kazi na Kocha Mserbia, Sredejovic
Milutin maarufu kama Micho lakini akafanya kazi na kocha mwingine wa zamani wa
Yanga, Tom Saintfiet katika klabu hiyo ya Free State ya Afrika Kusini lakini
baadaye timu ya taifa ya Togo.
0 COMMENTS:
Post a Comment