JOSE Mourinho, Kocha Mkuu wa Tottenham amesema kuwa hakuona msaada wa VAR kwenye mchezo wao dhidi ya Liverpool kwani kuna kadi nyekundu ya moja kwa moja ilipaswa itolewe kwa mchezaji wa Liverpool ambaye alicheza rafu mbaya kwa mchezaji wake.
Kwenye mchezo wa jana, Januari, 11, Liverpool ilishinda bao 1-0 lililopachikwa kimiani na Roberto Firmino dakika ya 37 akimalizia pasi ya Mohamed Salah ulikuwa na ushindani mkubwa kwa pande zote mbili.
Mourinho amesema kuwa ilipaswa kitendo cha Andy Robertson kitazamwe kwenye VAR ili apewe adhabu kutokana na kumchezea rafu Japhet Tanganga ila haikufanyika hivyo jambo ambalo halina maana ya uwepo wa huo mtambo inaonekana muda huo walikuwa wanakunywa chai.
Tottenham imepoteza mchezo huo ikiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani waTottenham Hotspurs ambayo ipo nafasi ya nane ikiwa na pointi 30 baada ya kucheza mechi 22 huku Liverpool ikiwa namba moja na pointi 61 imecheza mechi 21.
Mwamuzi wa mchezo huo Martin Atkison hakutoa nafasi kwa Spurs kucheza faulo wala kufanya marudio kwenye VAR jambo lililomkasirisha bosi huyo kwa kuwa kulikuwa na ulazima kwa msimamizi wa mitambo hiyo kusimamisha mechi na kutoa adhabu ya faulo kwao.
Hasira za Mreno huyo alikumbushia pia na mechi yake dhidi ya Chelsea wakati faulo ya nyota wake Son Heung-min ilirudiwa alipomchezea Antonio Rudiger wakati wakiambulia kichapo cha mabao 2-0 mbele ya Chelsea, Desemba 22,2019.
Robertson mwenye miaka 25, alikuwa msaada mkubwa kwa Liverpool wakati wakiibuka na ushindi huo wa kwanza kwenye uwanja mpya wa Tottenham na alicheza dakika zote tisini.
"Kiuhalisia walipaswa wamalize dakika tisini wakiwa na wachezaji 10 pekee kwenye mechi yao dhidi yetu, nadhani watu wa VAR muda huo labda walikuwa wanakunywa chai jambo lililowafanya washindwe kuona kadi nyekundu ambayo alistahili kupewa Robertosn ," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment