February 23, 2020


JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa timu ya Coastal Union amesema kuwa wachezaji wake wapo sawa na watapambana leo mbele ya Yanga kusepa na pointi tatu.

Mgunda amesema kuwa:-"Tulipomaliza mchezo wetu mbele ya Ruvu Shooting kazi ya kwanza ikawa kuyafanyia kazi makosa yetu na kupiga hesabu kwa ajili ya mchezo wetu unaofuata.

"Makosa yote yalikuwa juu yangu nimewaambia vijana namna ya kufanya matumaini yangu na timu kiujumla kuona inapata matokeo mbele ya wapinzani wetu mashabiki watupe sapoti,".

Mchezo wao utachezwa leo Uwanja wa Mkwakwani Tanga majira ya saa 10:00.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic