February 23, 2020



KOCHA Mkuu wa Kitayosce FC ya Tabora, Boniface Kiwale, amesema wamejipanga kucheza kufa au kupona dhidi ya Ndanda katika mchezo wa Kombe la FA utakaochezwa Februari 26, mwaka huu kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Kiwale amesema: "Nimekuwa nikiwafuatilia Ndanda kwa muda mrefu sana na sisi kama Kitayosce tumejiandaa kuhakikisha kwamba tunapata matokeo mazuri japokuwa mchezo huo utakuwa mgumu.

"Nimeona kwa mwezi huu Ndanda wamekuwa wakifanya vizuri kwenye ligi kuu hasa kwa michezo yao mitano iliyopita, lakini hilo halituogopeshi zaidi ya kwamba tunajipanga kupambana kufa au kupona ili tuweze kushinda."


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic